POLISI wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na kupiga risasi hewani kuwatawanya waandamanaji katika Jiji la Kampala wakipinga kukamatwa kwa mbunge wao, Robert Kyagulanyi mwanasiasa wa upinzani anayejulikana kwa jina la Bobi Wine.
Waandamanaji wamenachoma moto magurudumu ya magari, na kurusha mawe huku pia wakiweka vizuizi vya barabarani na kuimba “Nguvu ya watu. Nguvu yetu”.

Bobi Wine alikamatwa na kushtakiwa kwenye mahakama ya kijeshi wiki iliyopita kufuatia madai kuwa alikuwa anamiliki silaha kinyume cha sheria. Wengi wanayaona mashataka hayo kama yaliyochochewa kisiasa.

Wanajeshi na polisi wameonekana wakiwa juu ya magari wakipita kati kati mwa mji. Sehemu zingine za mji wa kampala maafisa wa usalama wamefyatua risasi hewania na kurusha vituo machozi kutawanya waandamanaji.

Misukosuko inaongezeka mjini Kampala kufuatia kukamatwa kwa mbunge Bobi Wine. Ripoti zimeibuka kuwa aliteswa akiwa mikononi mwa wanajeshi. Rais Yoweri Museveni amekana madai kuwa Bobi Wine alijeruhiwa.
Watu kadhaa wamekamatwa akiwemo mwandishi wa habari wa Reuters aliyekuwa akifuatilia ghasia hizo.

Wiki iliyopita Bobi Wine 32, na watu wengine walishtakiwa baada ya kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo eneo la Arua kaskazini mwa nchi. Polisi wanasema walikuwa wamewaongoza wafuasi wao kushambulia msafara wa Rais Museveni.
The post Mabomu Yarindima, Wananchi Wapinga Mbunge Kukamatwa appeared first on Global Publishers.