NEWS

29 Septemba 2019

Kim Nana Awaka Kisa Ujauzito

Mwanadada anayeuza nyago kwenye video za wasanii Bongo, Lilian Kessy ‘Kim Nana’ amewaka kwa mashabiki wake ikiwa ni muda mchache baada ya kutupia picha mtandaoni ikimuonyesha ni mjamzito.

 

Baada ya kuweka picha hiyo, mashabiki walimsema kuwa huenda mrembo huyo ni mjamzito hivyo ndio maana ameona awaonyeshee watu hususan mwanaume wake, Tonny Albert ‘Tbway’aliyeachana naye hivi karibuni.

 

Akipiga stori na Mikito Nusunusu mrembo huyo alisema muda ukifika watu watamuona huyo mtoto lakini siyo kwa sasa na hata kama akishika mimba sasa hivi siyo mbaya kwa sababu yeye ni mtoto wa kike na leba kuingia ni lazima.

 

“Jamani mimi si mtoto wa kike lakini? Sasa hata nikiwa na mimba kuna shida gani na kama kweli ninayo basi watu watamuona tu huyo mtoto,” alisema Kim Nana.

The post Kim Nana Awaka Kisa Ujauzito appeared first on Global Publishers.