NEWS

29 Septemba 2019

Makazi Mapya Ya Wema Balaa!

WAKATI wengine wakikalia umbeya; ‘mara ooh kafulia, hana makazi maalum ya kuishi, anatangatanga mitaani hadi kasitiriwa na mama yake’, staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ameibuka kivingine.

 

Taarifa ikufikie kuwa bidada huyo kwa sasa anaishi kwenye makazi mapya ya kifahari ile mbaya maeneo ya Ununio jijini Dar.

Baada ya maneno kuwa mengi mitaani kuwa hana pa kuishi, gazeti hili liliingia mzigoni ili kuthibitisha madai hayo ambapo lilianzia maeneo ya Bunju jijini Dar, lilikoelekezwa kuwa ndipo anapoishi Wema.

Kufuatia umaarufu wake, ilikuwa ni rahisi tu kujua kwani walipoulizwa watu wawili-watatu walisema anaishi Ununio.

“Anaishi maeneo ya Majumba ya Wasomali (Bunju), ukifika, ulizia nyumba anayoishi Wema, huwezi kupotea,” alisema dereva bodaboda.

 

Gazeti hili lilipofika maeneo hayo lilianza kuuliza ambapo safari hii lilielekezwa sehemu nyingine mbali na pale.

“Ni kweli Wema alikuwa anaishi maeneo ya huku, lakini alishahama, siku hizi anaishi Mtaa wa.. (anataja jina la mtaa), nadhani mkifika hapo ndipo nyumbani kwake,” alisema mama ntilie mmoja maeneo ya Majumba ya Wasomali, Bunju.

Gazeti hili lilifika kwenye mtaa huo na kuendelea kuuliza ambapo lilielekezwa tena sehemu nyingine na kuambiwa kuwa sehemu hiyo alishahama.

“Huku Wema hakukaa sana, alihama ila hakuhamia mbali sana, nendeni mbele, mtakuta kuna kibao kimeandikwa jina lake Wema Sepetu Street, hapo ndipo anapoishi.”

 

Mwandishi: Hee! Ina maana Wema kapewa mpaka mtaa?

Dada: Ndiyo amepewa, ndiyo maana wakaweka na kibao cha jina lake. Sasa mkifika hapo, ingieni (anaendelea kuelekeza) mtakuwa mmefika, nafikiri hata mkimuulizia hapo mtaoneshwa moja kwa moja nyumba yake.

 

Baada ya maelezo hayo, gazeti hili lilifanikiwa kufika eneo hilo na kukuta vijana wawili wakiwa dukani, ambapo baada ya kuwauliza walisita kwa muda kidogo kisha baadaye walielekeza anapoishi mrembo huyo.

Gazeti hili liliushuhudia mjengo anaoishi Wema ambao upo ushuani ambapo sauti za ndege tu ndizo zinazosikika.

 

Kingine mjengo huo upo kwenye mandhari ya kuvutia, uwanja mkubwa wa kupaki magari, miti na maua safi kwa ajili ya kupata hewa nzuri huku kukiwa na ulinzi kama wote kuanzia kamera na vifaa maalum.

Mbali na hayo yote gazeti hili lilifanikiwa kuona gari la Wema aina ya Toyota Crown Majesta likiwa limepaki uwanjani ndani ya fensi.

 

Waandishi wetu waligonga getini kwa muda mrefu, lakini hakutoka mtu yeyote kufungua.

Ilibidi gazeti hili ligonge kwa jirani yake ili kutaka kupata ukweli kama ni yeye anaishi pale au la.

Mwandishi: Hodiiii.

Jirani: (anafungua geti) Karibuni.

 

Mwandishi: Samahani tunaulizia kwa Wema, lakini tumefika hapa tunaona mageti mengi, sasa tumeshindwa kuitambua nyumba yake ni ipi.

Jirani: Ni ile pale (ananyoosha mkono wake kwenye geti la kijivu ambalo ndilo gazeti hili lilielekezwa.

Mwandishi: Asante sana, tunashukuru.

Jirani: Karibuni, anaingia ndani na kufunga geti lake.

STORI: Na Memorise Richard na Irene Marango, Risasi Jumamosi

The post Makazi Mapya Ya Wema Balaa! appeared first on Global Publishers.