NEWS

1 Oktoba 2019

JPM Amwondoa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi

magufuliRais Dkt. John Magufuli leo Oktoba 1, 2019 amefanya uteuzi na kuwahamisha vituo vya kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Manispaa na Wilaya, na pia amefanya uteuzi wa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal).

 

Rais Magufuli amemteua Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa Balozi na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kanali Ibuge anachukua nafasi ya Balozi Grace A. Martin ambaye atapangiwa majukumu mengine ya Kibalozi.

The post JPM Amwondoa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi appeared first on Global Publishers.