NEWS

26 Novemba 2019

UNO ya Harmonize kurudishwa Youtube, Producer aliyoifuta akubali yaishe


Mtayarishaji wa muziki nchini Kenya, Magix Enga aliyepelekea video ya wimbo wa Harmonize UNO kufutwa Youtube amekubali yaishe.



Kupitia ukurasa wake wa Instagram Magix Enga amefunguka kuwa UNO itarudi muda wowote kuanzia hivi sasa.

Ikumbukwe imechukua takribani wiki sasa tangu wimbo wa msanii kutoka Tanzania Harmonize kufutwa kwenye akaunti yake ya Youtube baada ya malalamiko kutoka kwa mtayarisha wa mzuki kutoka nchini Kenya Magix Enga akilalamika kuwa wimbo huo ulicopy beat ya wimbo wa msanii kutoka Kenya King Kaka DUNDAING.

Magix Enga kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii alimpa Harmonize wiki moja awasiliane nae na kutokana na maelezo yake Harmonize hakufanya hivi kwahiyo aliamua kuufuta wimbo huo kwenye mtandao wa Youtube na mara ya kwanza video ya UNO ilianza kufutwa na baadaye alitoa siku mbili kwa Harmonize kuwasiliana nae na baadaye Audio ya UNO pia ilipotea Youtube.

Kutokana na maelezo yake aliyofanya na Mzazi Willy wa Mseto Magix Enga alisema kuwa anachotaka yeye kutoka kwa Harmonize sio pesa bali ni heshima.

kupitia ukurasa wake wa Instgram ameandika hiki:-

“🇰🇪 🇹🇿 With #CLEMO @Ngomma ✌️Growth of East African music is bigger than all of us. And for this reason i have decided that I will release my copyright strike on Uno by Harmonize. I have decided to forgive the guy🇹🇿 Nitarudisha Uno by Harmoize Pale YouTube Wakati wowote #MagixEnga #DontSampleMagixEngaBeats to watch Full video go on YouTube .. don’t forget to subscribe 🇰🇪 🤴 ✌️“



Ingawa na yeye alilalamikiwa kuwa beat ya wimbo huo wa DUNDAING alisample kutoka kwa msanii wa Nigeria Olamide wimbo wa Matgbana alikataa na kusema project yake ilikuwa miaka miwili iliyopita na Olamide ilikuwa mwaka mmoja uliopita ila kiuhalisia Olamide aliitoa ngoma ya Motgbana august mwaka 2018 na yeye aliifanya ngoma DUNDAING mwaka huo huo ila ni mwezi october.