Cooper alimwomba uchumba EVE mwenye miaka 35 siku ya Christmas ya mwaka jana 2013 huko Edinburgh, Scotland walipoenda kusheherekea sikukuu.
Kama wafanyavyo wasichana wengine wanapoingia katika status ya ‘uchumba’, EVE aliionesha pete yake ya uchumba ya almasi kupitia Instagram na kuandika,
“Asante kwa kila mmoja kwa pongezi zenu za engagement! Tulitaka kusheherekea na familia yetu na marafiki kwanza kabla ya kutangaza”.
Eve akiwa na mama yake na kaka yake, tayari pete ya uchumba ikiwa kidoleni
Baadaye mchumba wake naye aliandika kupitia ukurasa wake “Yes it’s official…I asked the question…and she said YES! WAHOOO! we’re getting married!”.
Hii itakuwa ni ndoa ya kwanza kwa Eve, wakati mume wake mtarajiwa tayari ana watoto wanne waliopatikana katika ndoa zake zilizopita.