NEWS

15 Januari 2014

Mabadiliko ya Gmail yazua wasiwasi

Wateja wa huduma za barua pepe za Gmail hivi karibuni wataweza kutuma ujumbe moja kwa moja katika akaunti nyinginezo za Gmail licha ya watumiaji kutofahamiana.

Mpango huu mpya utawafaidi watumiaji wote wa Gmail na Google+, mtandao mkubwa wa kijamii wa Google.


Mabadiliko haya hata hivyo yamesabisha wasiwasi mkubwa miongoni mwa wanaotetea usiri wa taarifa za watu kwenye mitandao, ambao wanasema wateja wanaweza kupata barua pepe kutoka kwa watu wasiowafahamu ambao hata wanaweza kuwa majambazi.

Hata hivyo Google inasema kuwa itarahisisha mawasiliano kwa njia hii kati ya watumiaji wa Gmail.

Lakini mwanaharakati mmoja amesema mabadikilio hayo ya Google ni ya kutia wasiwasi kwa sababu huenda mtu usiyemjua akaanza kukutumia barua pepe kwa nia mbaya.

Wateja wa Gmail wataona orodha ya anwani za marafiki zao na za watu wasiowajua kwenye akaunti zao pindi watakapoanza kutuma ujumbe wao.

Mabadiliko haya yalitangazwa na meneja wa kampuni hiyo Alhamisi David Nachum, aliyesema kuwa mabadiliko haya yatarahisisha watumiaji wa Gmail kujuana vyema.