NEWS

13 Januari 2014

Mtoto wa Whitney Houston, Bobbi Kristina afunga ndoa na kaka yake...

Hatimaye mtoto wa marehemu Whitney Houston na mwimbaji Bobby Brown aitwaye Bobbi Kristina Brown na aliyekuwa mchumba wake (kaka yake) Nick Gordon wame ‘tie the knot’!

Haikufahamika mpaka Bobbi alipotweet furaha aliyonayo ya kuwa mke wa chaguo la moyo wake Gordon.’#HappilyMarried So #Inlove if you didn’t get it the first time that is,’ Alitweet Bobbi alhamisi ya wiki hii pamoja na picha inayoonesha mikono ya wawili hao ikiwa na pete za ndoa vidoleni mwao.



Bobbi mwenye miaka 20 alitangaza juu ya uchumba wao mwezi Octoba (2012), kabla ya kuachana muda mfupi baadaye. Walikuja kurudiana tena na kurudisha uchumba wao mwezi July (2013).Uhusiano wa wawili hao umekuwa ukichukuliwa kama wa kaka na dada kutokana na kwamba Nick (24) alilelewa na marehemu Whitney kama mwanaye wa kumzaa kwa kipindi kirefu kiasi cha Bobbi na yeye kuwa kama ndugu wa damu.

“YES, we me nick are engaged”. Aliwahi kujitetea Bobbi, “I’m tired of hearing people say “eww your engaged to your brother” or “if Whitney was still alive would we be together or would she approve of this,”. Alisema katika ukurasa wake wa facebook mwaka jana.

Source:Daily Mail