Katika mazishi hayo yaliyofanyika leo kijiji kwake Magunga jimbo la Kalenga wananchi mbali mbali walionyesha kujipanga barabarani kutoka Manispaa ya Iringa hadi kijijini kwake huku wakiupungia mkono msafara wa rais Kikwete na baadhi yao wakilazimika kutumia usafiri wa baiskeli na pikipiki kwenda katika mazishi hayo.
Alisema katika uhai wake kabla ya kifo chake ikiwa ni siku tano kabla Dr Mgimwa alimwita na kumtaka kufikisha shukrani zake kwa Rais Kikwete kwa kumtembelea mara mbili Hospital alipokuwa amelazwa pamoja na spika wa bunge Anne makinda .
Pia alisema kuwa alieleza dhamira yake ya kuwatumikia wana Kalenga na kusema zawadi kubwa ni msaada wa bati zaidi ya 2000 kwa wananchi hao ili kuendeleza ujenzi wa shule na vituo vya afya jimboni.
"Baba kabla ya kufa aliniachia wosia huo juu ya wana Kalenga kwa kuwashukuru kwa ushirikiano wao na kutoa bati ila alipenda kuona Kalenga inakuwa na maendeleo zaidi"
Kwa upande wake waziri Mkuu Pinda alisema kuwa serikali imepata pigo kubwa juu ya kifo hicho na kuwa bado serikali itaendelea kuwa karibu na familia ya Dr Mgimwa na pale penye tatizo isisite kuwasiliana .
Hata hivyo Rais Kikwete hakupata kuzungumza chochote katika msiba huo zaidi ya kuweka mchanga na shada la maua pamoja na kuwapa mkono ndugu wa Dr Mgimwa .
Spika wa bunge Anne Makinda alisema kuwa bunge limempoteza kiongozi na mbunge aliyependa kutumia nafasi yake kwa ajili ya Taifa na kuwa kamwe mchango wake hawataacha kuukumbuka.