Vitu hivyo ni pamoja na miwani ya jua inayodaiwa alikuwa ameivaa siku hiyo kabla ya ajali, chombo cha kuzimia moto (fire extinguisher) kilichotumika kujaribu kuuzima moto baada ya ajali.
Kwa mujibu wa New York Daily, mtaalam wa kampuni ya minada BidAMI.com amesema mtu aliyewapelekea vifaa hivyo alidai kuwa aliviokota vichakani karibu na eneo ilipotokea ajali, na alipojaribu kuwasiliana na familia ya Walker hawakuonesha nia ya kuvichukua.”We photo-matched them to the one’s Paul was wearing [that day].”
Sehemu ya fedha zitakazotokana na mnada wa vifaa hivyo zitapelekwa savethemustangs.org kwaajili ya charity.
