
May 8 mwaka huu iliripotiwa kuwa Apple inampango wa kuinunua kampuni hiyo kwa dola bilioni 3.2.
Waanzilishi wa Beats producer mkongwe wa Hip Hop Dr. Dre na mwanzilishi wa Interscope Jimmy Iovine watapewa vyeo vya juu katika kampuni ya Apple, ambavyo hata hivyo havikutajwa moja kwa moja katika tangazo hilo.
Dre na Lovine walinzisha Beats Electronics mwaka 2008 na kwa wakati huo walikuwa wakitengeneza headphones peke yake, lakini kwa sasa pia wana mtandao wa kustream muziki.
Deal ya Apple kuinunua kampuni ya Beats Electronic inatarajiwa kukamilika September 30 mwaka huu.

