NEWS

25 Juni 2014

Inasemekana hawa ndio Mastaa wa kibongo waliowazidi umri wapenzi wao

Mara nyingi tunaishia kusikia rumors tu, kuwa msanii fulani amemzidi umri mpenzi wake na mara nyingi mwisho wa siku rumors zinabaki rumors tu, hadi pale wawili watakapofunguka wenyewe juu ya suala hilo, basi hii ni list ya wasanii wachache tu maarufu na wenye majina hapa town, ambayo inasemekana kuwa wamepigana gape kiumri.









Diamond Platnumz Vs Wema Sepetu.






Kutokana na wikipedia Diamond Platnumz amezaliwa mwaka 1989 wakati Wema Sepetu amezaliwa mwaka 1988, wawili hawa walioshibana wamepishana miezi michache tu, huku Wema Sepetu ndio inaonyesha amemuacha Diamond Platnumz kwa miezi michache tu. Hii ni moja ya couple maarufu sana Africa, huku kila mmoja akiwa ana-shine bila kutegemea mgongo wa mwenzie, Diamond akiwa anakimbiza kwenye anga za muziki wakati Wema akiwa ndio actress maarufu anayependwa zaidi na watu na anayeongoza kuwa na mashabiki wengi East Africa.


Shilole Vs Nuh Mziwanda.





Rumors had it kuwa Shilole amempiga gape(amemuacha kiumri) Nuh Mziwanda, na siku ilipofika wawili hao walipoamua kufunguka juu ya mapenzi yao, story zilizagaa kuwa Shilole amepata serengeti boy, ingawa hadi hivi sasa haijulikani wameachana kiumri kwa miezi au miaka mingapi.



Irene Uwoya Vs Msami.




Ni juzi kati tu, wadau walibaini kuwa wawili hawa wapo katika mapenzi moto moto, na mwisho wa siku ikabidi wafunguke na ku-confirm ukweli huo kuwa wao ni wapenzi kwa sasa, ila rumors had it kuwa Irene Uwoya amemzidi umri Msami, na watu kuanza kuamini rumors hizo hadi pale Msami juzi kati alipoamua kufunguka kuwa yeye amemzidi umri Uwoya kwa miezi mingi tu, ingawa hakufunguka kuhusiana na miezi mingapi.


"Ila juu ya yote Mapenzi hayaangalii Umri, Pesa wala Mali" Je unahis mapenzi ya mastaa hawa wakibongo yatadumu?