Nick Mutuma na Jokate Mwegelo
Mjenzi wa ufa uliokuwa umebomoka kwenye moyo wa Jokate kutokana na mahusiano yake yaliyopita (Hasheem Thabeet na Diamond), anaweza akawa ameshapatikana. Naye si mwingine ni muigizaji wa kipindi cha MTV Shuga na mtangazaji wa redio, Nick Mutuma.
Tangu aende Nairobi Kenya kikazi, Jokate na Mutuma wamekuwa karibu kiasi cha kuzalisha cheche za uwepo wa uhusiano kati yao. Kupitia Instagram, Mutuma alipost selfie akiwa na mrembo huyo aliyemlalia kifuani kama msichana afanyavyo kwa boyfriend wake.
Picha hiyo ilivuta macho na comments za wengi kwenye mtandao huo huku wengi wakisema wanapendeza kuwa pamoja.
“I pray u b a couple..those kids u’ll get tho’ lol @nickmutuma , @jokatem,” ameandika mmoja na mwingine kuchombeza: That is one cuuuute couple aaaaaaww!!!!
Jana pia Nick alipost picha hii ya TBT: