Akizungumza na gazeti hili mapema juzi, Nay mkali wa nyimbo za Nakula ujana na Muziki Gani, alisema mabinti wengi wanacheza filamu siyo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha, bali wanafanya hivyo ili kuuza sura ambayo baadaye huitumia kwa ajili ya kujiuza ili kujiingizia kipato.
“Mimi kila kitu ambacho huwa ninakiimba huwa kina ukweli ndani yake na niko tayari kwa mtu ambaye atahisi nimemuonea tutafikishana popote pale, nilishawahi kushuhudia mabinti wa bongo movie wakinunuliwa na wageni wanaokuja kutoka nje ya nchi,” alisema Nay.