Mwanamitindo afanyae kazi zake za mitindo nchini Marekani Flaviana Matata, yuko nchini kwa ajili ya kufanya kazi za kijamii kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation kupitia mradi wa Back to school project/FMFstationary kit ambao unafadhiliwa na mfuko wa penseni PSPF.
Baada ya mwezi January Flaviana kugawa vifaa shule za msingi za jijini awamu hii ameenda mkoani Lindi na kufanikiwa kugawa shule za Msingi Mtua na Chemchem ziliyopo Nachingwea pamoja na shule za msingi Litingi na Mnengulo zilizopo Lindi.
Bado wanaendelea kugawa vifaa hivyo kwa shule za msingi mikoa mingine. “Hadi sasa tumeshagawa vifaa kwa watoto 700 na bado kuna kits 800 vitasambazwa Tunduma ,Tunduru na Monduli,” alisema Flaviana.
Flaviana alitoa shukran kwa PSPF kwa kudhamini huu mradi na akasisitiza makampuni na mashirika kujaribu kuwezesha elimu kama hali halisi inavyoonekana kwenye picha hadi leo kuna wanafunzi wanasoma chini na mti, na walio madarasani,madarasa ni mabovu na hayana madawati.
Flaviana Matata aliongozana na Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin pamoja na wafanyakazi wa PSPF katika zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.