NEWS

2 Septemba 2014

Wema Sepetu: Simlishi Mpenzi Wangu Diamond Viporo na Wala Siweki Chakula Kwenye Hot Pot 'Pata Michapo'

Mahaba Niue, Mahabati Beautiful Onyinye wa Bongo,Wema Sepetu ‘ Madam’ amedhihirisha kuwa
yeye ni mwanamke tayari wa kuwekwa ndani baada ya kusema anajitahidi kila siku katika
suala la mapishi ili asimlishe viporo Akipiga domo na paparazi wetu, Wema
alisema kama mwanamke anajua thamani ya mwanaume siku zote hata kama ‘ baby’ wake
atarudi usiku , lazima aingie jikoni kupika na haweki chakula kwenye ‘ hot pot ’ .



“Siku zote si kwamba najisifia ila kwa jikonindiyo mwenyewe sasa kwa nini nipike chakula halafu niweke kwenye hot pot ?  Kwangu siruhusu kabisa itokee , ” alisema
Wema .