NEWS

21 Oktoba 2014

Umeisikia mpya kuhusu Ebola ndani ya Marekani? Stori kamili iko hapa

Ni kawaida kusikia mtu kapewa ‘a.k.a’ ambayo lazima kuna kitu kilichopelekea akapewa a.k.a hiyo, huenda ikawa ni muonekano wake, tabia, mavazi ama kitu chochote kile kinachohusiana na yeye.

Watu wamekuwa wakitoa ‘a.k.a’ hata kwa vitu vingine pia, lakini kali ni hii kutoka Marekani, ambapo ripota wa kituo cha televisheni cha CNN alitoka kali baada ya kutoa a.k.a ya ugonjwa wa Ebola, kwa kuuita “Fear-bola”



Mel Robbins amenukuliwa katika ukurasa wa mtandaoni wa kituo hicho akisema; “Fear-bola inashambulia sehemu ya ubongo inayohusika na kuwaza mambo ya busara”

Mtangazaji huyo aliongezea kuwa ‘Fear-bola’ ilianza pale ilipogundulika wauguzi 2 walipata maambukizi hayo huko Dallas, na baadaye ikatanda ‘ugonjwa wa hofu’ kila kona ya Marekani.