Masuala yoyote yanayohusiana na uchawi wa ushirikina katika michezo yoyote hayaruhisiwi, hii ni ili kuhakikisha kuwa pande zote mbili zinazoshindana katika mchezo husika zinakuwa na uwanja sawa ili kumpata mshindi kwa haki.
Lakini huenda umekuwa ukisikia masuala ya kishirikina kwenye mpira ya hukuwahi kushuhudia, sasa sakata hili lililotokea katika Ligi Kuu nchini Rwanda litakushangaza na kuona nguvu ya ushirikina katika mchezo.
Katika mchezo uliochezwa kati ya Mukura Victory na Rayon Sports katika uwanja wa Huye ambapo hadi dakika nne za nyongeza Mukura walikuwa wakiongoza, mshambuluaji wa Rayon Sport alifanya kitendo cha kishirikina katika goli la Mukura na kufanikiwa kuisawazishia klabu yake.
Katika video ya mchezo huo uliorushwa na Azam Tv, mshambuliaji huyo alifanya kitendo hicho na sekunde chache tu alifunga goli. Moussa Camara alikosa nafasi ya kufunga goli kisha akainama na kuchukua kitu katika lango la Mukura na kuanza kufukuzwa na mlinda mlango.
Sekunde chache baadae Camara anaifungia timu yake goli na kufanya mchezo kuwa 1-1.
Hapa chini ni video ya tukio hilo.
Mshambuliaji wa Rayon Sport ya Rwanda, Moussa Camara afanya kitendo cha kishirikina na kuisawazishia klabu yake dhidi ya Mukura Victory. http://pic.twitter.com/vvGc0yjIuL
— Swahili Times (@swahilitimes) December 29, 2016
Shirikisho la Soka la Rwanda limesema kuwa kama timu ya Rayon Sport itabainika kuwa ilihusika na kitendo hicho itatozwa faini ya milioni 2.9 kwa fedha za Rwanda (TZS milioni 7.7) pamoja na kupokwa alama za mchezo huo.
Aidha mchezaji huyo ametozwa faini ya fedha za Rwanda (Franc) 100,000 ambayo ni sawa na 264,171 fedha za Tanzania.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini Rwanda, Vedaste Kayiranga amesema kuwa shirikisho hilo halina vifungu vyovyote vya sheria vinavyozuia matumizi ya uchawi katika mchezo sababu hakuna sehemu yoyote duniani ambapo imethibitishwa kuwa uchawi/ushirikina unaweza kuamua matokeo ya mchezo.
Aidha alisisitiza kutokana na ugomvi ambao huibuka baina ya wachezaji kwa tuhuma za uchawi, wameamu kutunga vifungu hivyo.
The post Video: Mchezaji akifanya kitendo cha kishirikina katikati ya mchezo na kufanikiwa kufunga goli appeared first on SWAHILI TIMES.