Rais Dkt Magufuli yupo mapumzikoni kijijini kwake Lubambangwe, Chato Mkoani Geita.
Aidha, Rais anatarajia kufanya ziara Mkoani Kagera kuanzia tarehe 06 hadi 09 Novemba, 2017.
Dhumuni la ziara ya Mhe. Rais Magufuli ni kuwatembelea wananchi wa Mkoa wa Kagera pia kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani hapa.
Vilevile Mhe. Rais Magufuli atapata fursa ya kuongea na wananchi kwenye Mkutano wa Hadhara Uwanja wa Ndege wa Bukoba.