NEWS

27 Februari 2018

Benki ya NMB yafungua tawi jipya Ruaha, Iringa

Zoezi za kukata utepe kama ishara ya uzinduzi likifanyika.

Baada ya zoezi la kukata utepe likimalizikia

 

BENKI ya NMB Tanzania imezindua tawi jipya Ruaha ambalo limeanzishwa kwa lengo la kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi wa mkoa wa Iringa.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa NMB Bw. Abdulmajid Nsekela alisema,” Benki ya NMB imeendelea kuwa benki yenye mtandao mpana zaidi wa matawi na ATM; tawi hili likiwa ni la 214 na ATM zaidi ya 800 nchi nzima huku ikiwa na mawakala wanaotoa huduma za NMB zaidi ya 4000 nchi nzima huku ikijivunia wateja wake zaidi ya milioni 3.

 

“Mafanikio haya yasingeelezwa leo kama si kuaminiwa na wateja wetu ambao miongoni mwao ni wana Ruaha na Iringa kwa ujumla kuwa benki wanayoipendelea zaidi na hivyo kuwa ni benki yenye mafanikio makubwa zaidi nchini.”

Pamoja na ufunguzi wa tawi hilo, pia benki ya NMB ilitoa msaada wa milioni 5 ambazo zitaelekezwa katika sekta ya afya na elimu, ambapo Nsekela aliitaka serikali kusema ni maeneo gani ingependa pesa hiyo itumike.

 

The post Benki ya NMB yafungua tawi jipya Ruaha, Iringa appeared first on Global Publishers.