NEWS

22 Februari 2018

Halotel yafikisha 10% ya wateja wote wa simu nchini

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano , Mhina Semwenda (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

 

 

KAMPUNI ya Halotel Tanzania imetangaza kuendelea kupata mafanikio na kuongezeka kwa kasi ya ukuaji katika kipindi cha robo tatu ya mwisho ya mwaka 2017 na kufikia asilimia kumi 10 ya idadi ya wateja wote wa mitandao ya simu takwimu zinaonesha.

 

Katika Takwimu hizo za hivi karibuni, zilizochapishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Tanzania (TCRA), zinaonyesha kwamba namba ya wateja wa Halotel imekuwa na kufikia milioni  nne hadi Desemba 2017 katika soko la ushindani ambapo makampuni saba ya simu za mikononi, yamekuwa yakishindana katika kusajili wateja million 40 kwa kadi za simu.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano , Mhina Semwenda amesema, haya ni mafanikio makubwa kwa kampuni ya Halotel ambapo ndani ya miaka miwili wameweza kufikia wateja wapatao  Milioni tatu na laki nane hadi kufikia Septemba 2017.

 

Pamoja na wateja  hao sehemu ya soko la Halotel ilifikia kiwango cha tarakimu mbili ya asilimia 10 kutoka asilimia tisa mwaka 2017. Hii ina maana kwamba kampuni hiyo iliyoanza kutoa huduma miaka miwili iliyopita miaka miwili imeweza kupita baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa kwenye soko kwa zaidi ya miaka kumi.

 

Vile vile, kampuni imeweza kuongeza sehemu ya soko katika  huduma za kifedha kwa njia ya simu ( Halopesa)  kwa asilimia nne wakati wa robo ya mwisho ya mwaka 2017, ambayo imekua kutoka kwa asilimia mbili tu kwa Septemba mwaka 2017 ilikuwa na jumla ya milioni moja katika huduma yake ya halopesa hadi kufikia januari mwaka huu.

 

Ukuaji huu mkubwa umekuwa ni mahsusi kwa ukuaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu huku huduma ya HaloPesa kuwa miongoni mwa huduma za kifedha zinazotolewa na makampuni ya simu.

 

Uongozi wa kampuni hiyo ya simu umeeleza kuwa mafanikio haya ni sehemu ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni hiyo sambamba na mazingira bora ya uwekezaji yaliyowekwa na mamlaka husika.

 

“Tunajivunia kiwango cha ukuaji wa haraka na mkubwa zaidi ambao tumepata kuushuhudia miongoni mwa makampuni ya simu nchini na Afrika kwa ujumla. Tumewekeza kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka miwili na ukuaji huu ni ushahidi tosha wa uwekezaji huu,” alisema Mhina.

Hivi karibuni waandaaji wa tuzo za Kimataifa kwa kampuni mbalimbali duniani (Stevie Awards 2017) waliweza kutambua kiwango cha ukuaji wa kampuni ya Halotel Tanzania  na kuitunuku tuzo ya kimataifa ya kibiashara iliyotambulika kama “Kampuni inayokua kwa kasi zaidi kibiashara katika ukanda wa nchi zilizo Mashariki ya Kati na Afrika kwa mwaka 2017.

 

Kampuni hiyo, kwa mujibu wa Semwenda imewekeza dola milioni 800 (takribani Sh1.7 trilioni) katika upanuzi wa mtandao na kuboresha huduma za mawasiliano nchini Tanzania tangu Oktoba 2015, huku wakiweka malengo ya kuanzisha huduma za 4 G LTE pamoja na huduma nyingine za Mawasiliano.

 

The post Halotel yafikisha 10% ya wateja wote wa simu nchini appeared first on Global Publishers.