NEWS

20 Februari 2018

KUMBE FID Q, MPENZI WAKE WAMEUNGANISHWA NA PILAU

 

 

MKALI wa Hip Hop ambaye anakimbiza kwenye gemu kwa sasa na ngoma ya Fresh Remix, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, hivi karibuni ameweka wazi kuwa aliunganishwa na pilau na mpenzi wake aitwaye Karima, ambaye ni mkazi wa Tanzania na Uingereza.

Akichonga na Full Shangwe, Fid alisema mpenzi wake huyo baada ya kufahamiana miaka miwili iliyopita, sikukuu moja ya Eid mwanadada huyo alimtumia picha ya pilau alilokuwa amepika na akamuomba siku moja ampikie pilau hilo.

“Kwa hiyo hilo lilikuwa deni, baada ya kurudi Bongo, dada huyu siku moja alitimiza ahadi yake ya kunipikia pilau na uhusiano wetu ndiyo ukawa umeanzia hapo. Tuna mipango mingi ya kuishi pamoja kwa hiyo mengine Mungu akipenda yatajulikana baadaye,” alisema Fid Q.

 

Stori: Boniphace Ngumije

The post KUMBE FID Q, MPENZI WAKE WAMEUNGANISHWA NA PILAU appeared first on Global Publishers.