NEWS

21 Februari 2018

MGUU WA MTOTO WANASA KWENYE NGAZI ZA UMEME AIRPORT

 

 

Mtoto Julian ambaye mguu wake ulinaswa kwenye ngazi za umeme kwenye uwanja wa ndege wa Vancouver, Canada. Mama yake, Andrea Diaczok, ametoa wito kwa wazazi kuwa macho na watoto wao katika sehemu hizo.

Kiatu cha Julian kikiwa katika mashine za ngazi za umeme kilipokuwa kimenasa.

Julian akiwa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu, kinyume na woga wa wazazi wake ambao walifikiri huenda mguu wake ungekatwa.

Wazazi wa Julian wakifurahi naye baada ya matibabu ya mguu wake ambayo yalichukua wiki kadhaa.

 

MTOTO Julian mwenye umri wa miaka miwili alijikuta akivunjwa mifupa ya mguu wake uliponasa kwenye ngazi za umeme katika kiwanja cha ndege cha Vancouver, Canada.

 

Julian alikuwa na wazazi wake, Andrea Diaczok, mama yake,  na baba yake, Jeff Lee walikuwa wakirejea mjini Calgary wiki iliyopita kutokea Vancouver.  Mguu wa mtoto huyo ulikwama pembeni kati ya ngazi na vyuma vinavyozungusha mikanda inayopandisha abiria.

 

“Mguu wake ulipotea kabisa kwenye mkanda unaozunguka,” Diaczok, alisema na kuongeza kwamba kuona hivyo alipiga kelele kwa nguvu.

 

“Mtambo huo uliukunja mguu wake na kuvunja mifupa ya mguu ambapo kiatu chake kilipotelea ndani ya mkanda huo wenye kuzunguka,” alisema.

 

Kiatu cha Julian kilikuwa kimebanwa kwenye mkanda huo na ilibidi wafanyakazi wa uwanjani hapo na wapita njia kumng’oa mahali hapo aliponasa.

 

Diaczok na Lee ambao ni wafanyakazi katika fani ya afya, walikuwa wamejitayarisha kwamba mwanao angekatwa mguu. Hata hivyo, madhara hayakuwa makubwa sana, kwani mbali na mifupa iliyokuwa imevunjika na miteguko kadhaa, madaktari waliweza kuhakikisha mtoto huyo anapata matibabu ambayo hayakuwalazimisha kuukata mguu huo.

 

 

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA YA HABARI

The post MGUU WA MTOTO WANASA KWENYE NGAZI ZA UMEME AIRPORT appeared first on Global Publishers.