NEWS

24 Februari 2018

MTOTO WA RAY ALAMBA SHAVU NMB

MTOTO wa Staa wa Filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’, aitwaye Jarden Kigosi, amepata shavu la Ubalozi wa Benki ya NMB, ambapo amemfungulia akaunti kwa ajili ya kuhakikisha wanamwekea fedha zitakazokuja kumsaidia baadaye kwenye masomo yake na maisha ya baadaye.

Akizungumza na Global Publishers wakati wa kumfungulia akaunti hiyo, Makao Makuu ya Benki ya NMB, Posta jijini Dar, Ray alisema kuwa, amefurahishwa na hatua ya benki hiyo kumtumia mwanaye kama mmoja wa mabalozi jambo ambalo hata yeye alikuwa akilitamani sana japo hakujua wapi angeweza kumfungulia akaunti kwa ajili ya maisha yake ya badaye.

 

“Niwaombe tu mastaa wenzangu kuwa, suala la mtoto kumfungulia akaunti benki ni ya muhimu sana kwani sisi wazazi tupo leo lakini hatujui kesho yetu itakuwaje?

“Ili usimnyime haki ya maisha mazuri mwanao hapo baadaye, basi ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha anamfungulia akaunti mwanaye ila hata asipokuwepo ataweza kusoma bila shida,” alisema Ray.

Ray aliambatana na mzazi mwenzake ambaye pia ni msaniiwa Bongo Movies, Chuchu Hans katika utambulisho wa mtoto wao Jarden kama Balozi wa NMB.

Musa Mateja

 

The post MTOTO WA RAY ALAMBA SHAVU NMB appeared first on Global Publishers.