NEWS

26 Februari 2018

Polisi: Wema Aliniambia Anatumia Bangi Kujistarehesha Tu!

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeendelea na kesi inayomkabili muigizaji Wema Sepetu ambapo Ofisa wa Polisi WP Mary ameieleza mahakama kuwa mnamo Februari 4, 2017 Wema alimwambia anatumia bangi kwa ajili ya starehe na si kuuza

 

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba na Wakili wa serikali Costantine Kakula, Mary ambaye ni shahidi wa tatu katika kesi hiyo amedai kuwa wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwa Wema, Bunju Basihaya, Dar, alimuuliza Wema kuhusu tuhuma zinazomkabili kwamba anahusika na biashara ya dawa za kulevya au kutumia ambapo alijibu “Sijishughulishi na kuuza ila natumia bangi kama starehe”.

 

Sahidi huyo amedai baada ya kumuuliza Wema alimwambia mara yake ya mwisho kuvuta bangi ilikuwa Jumatatu ya wiki hiyo. Hata hivyo baada ya kufika nyumbani Wema alimpigia simu dada yake Nuru Sepetu ili awepo wakati wa kufanya ukaguzi huo ambapo dada yake alifika.

Shahidi anaeleza;

“Wakati Wema anampigia simu dada yake alitoka dada mmoja wa kazi kumfuata mjumbe ambapo alikuja naye na kujitambulisha kwa jina la Steven Ndaho. Baada ya Nuru kufika aliwapekua wote kabla ya kuingia ndani na upekuzi ulipokamilika tulirudi Central.

“Mnamo Februari 8,2017 saa nne asubuhi, Mary nilipewa maelekezo na Inspekta Willy niende na Wema kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukuliwa sampuli ya mkojo.”

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hadi Machi 12 na 13, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea tena na ushahidi.

The post Polisi: Wema Aliniambia Anatumia Bangi Kujistarehesha Tu! appeared first on Global Publishers.