NEWS

17 Februari 2018

Tazama Matokeo ya Uchaguzi Kinondoni Kutoka Vituo Mbalimbali

HAPA nimekuwekea matokeo ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni yameanza kubandikwa nje ya vituo vya kupigia kura yakionyesha mgombea wa CCM, Maulid Mtulia akiongoza katika baadhi ya vituo.

Katika matokeo hayo, Mtulia anafuatiwa kwa karibu na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu huku wa CUF,  Salum Rajab Juma akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.

Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo;

Kituo cha Mashuka namba mbili Kata ya Tandale

Mtulia kura 45

Mwalimu 16

Salum Juma kura 7

Wagombea wengine tisa wa vyama vingine wakipata kura sifuri.

Katika kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama C3

Matulia amepata kura 23

Mwalimu 24

Mgombea wa CUF akipata kura 1 na Mohamed Majaliwa wa NRA kura 1.

Kituo hicho kina wapigakura 373 ila waliopiga kura ni 49.

Kituo cha Kijitonyama C2,

Mwalimu kura 18

Mtulia 18

wagombea wengine wakipata sifuri.

Kituo cha kijitonyama Shule ya Msingi C1,

Mtulia amepata kura 29,

Mwalimu kura 34

Juma wa CUF kura 1.

Kituo cha Ofisa Mtendaji wa Kata A-4, Kata ya Hananasifu

Mtulia kura 38,

Mwalimu kura 29 na Juma 2.

Katika Kituo cha Ofisa Mtendaji wa Kata C2,

Kata ya Hananasifu;

Mwalimu kura 43

Mtulia kura 34.

Kituo cha Ofisa Mtendaji wa Kata B-1, Kata ya Hananasifu;

Mtulia kura 42,

Mwalimu 32

Wagombea wa CCK na TLP wakipata kura moja kila mmoja.

Kituo cha Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa B4 kilichopo Kata ya Hananasifu;

Mtulia amepata kura 31

Mwalimu kura 37,

Juma 1

Mgombea wa Tadea kura 1.

Kituo cha Kisutu A-2 Kata ya Hananasifu;

Mtulia kura 48,

Mwalimu 39.

Kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kisutu A-3 Kata ya Hananasifu

Mwalimu kura 29

Mtulia kura 32

Juma kura 1.

Kituo cha Leaders Club Frat-3 Kata ya Kinondoni

Mtulia kura 35

Mwalimu 27.

Kituo cha Ofisi ya Mtendaji Mtaa B-1 Kata ya Hananasif

Mtulia amepata kura 42

Mwalimu kura 32.

Kituo cha Hananasif A1 Kata ya Kinondoni

Mtulia amepata kura 37,

Mwalimu 23

Juma 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama Kata ya Kijitonyama

Mwalimu amepata kura 19

Mtulia kura 19.

Kituo cha Ofisi ya Ardhi-2 Kata ya Kinondoni

Mwalimu amepata kura 23, Mtulia 19.

Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama A-1

Mtulia kura 25

Mwalimu kura 35.

Kituo cha Idrisa 6 Kata ya Magomeni

Mtulia amepata kura 58

Mwalimu kura 21.

Kituo cha Idrisa 3 Kata ya Magomeni,

Mwalimu amepata kura 180

Mwalimu kura 36

Juma 3.

Kituo cha Idrisa 1 Kata ya Magomeni

Mtulia kura 26

Mwalimu kura 21

Juma 3.

Kituo cha Idrisa 2 Kata ya Magomeni

Mtulia amepata kura 44

Mwalimu 23

Juma 3.

Kituo cha Ofisi ya Aweo-5 Kata ya Makumbusho

Mtulia amepata kura 42

Mwalimu 20

Juma 2.

Kituo cha Weo Kata ya Makumbusho

Mtulia amepata kura 54

Mwalimu 36

Juma 1

Johnson Mwangosi wa Sau 1.

Matokeo zaidi yataendelea kukujia hapahapa

The post Tazama Matokeo ya Uchaguzi Kinondoni Kutoka Vituo Mbalimbali appeared first on Global Publishers.