NEWS

27 Februari 2018

Zidane Ampiga Chini Ronaldo

KOCHA wa Real Madrid ya Uhispania, Zinedine Zidane amemwacha Cristiano Ronaldo katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza leo usiku dhidi ya Espanyol kwenye Ligi Kuu nchini humo, La Liga.

 

Zidane amesema Ronaldo hatacheza kwa sababu ameamua kumpumzisha huku mapumziko hayo yakitafsiriwa kama amemuacha ili asubiri mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG utakaopigwa Machi 6.

 

Ronaldo amepumzishwa mara ya mbili ndani ya mechi tatu ambapo Zidane alifanya hivyo katika mechi ya ligi kuu katikati ya wiki iliyopita dhidi ya Leganes.

 

Hata hivyo, nafasi yake huenda akaanza Marco Asensio ambaye ameonekana kuwa na mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji, akiungana na Gareth Bale  na Karim Benzema kwenye safu ya ushambuliaji.

 

Madrid itasafiri katikati ya juma lijalo hadi nchini Ufaransa kwenye mchezo wa UEFA dhidi ya PSG huku ikiwa mbele kwa mabao 3-1 iliyoyapata kwenye uwanja wake wa Santiago Bernabeu.

The post Zidane Ampiga Chini Ronaldo appeared first on Global Publishers.