NEWS

16 Machi 2018

JK Atoa Kauli kwa Jeshi la Polisi

kikwete1

RAIS Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’ amefunguka na kulipongeza jeshi la polisi Tanzania kwa kufanikisha kukamatwa kwa watu ambao walikuwa wakitumia vibaya majina yake, mkewe na mtoto wake kuwaibia Watanzania. 

 

Jeshi la Polisi nchina Tanzania limewatia mbaroni wanawake watatu ambao walikuwa wakitumia majina ya Rais Kikwete mkewe kwa kuiba fedha za wananchi kwa kuwalaghai kuwa wanatoa mikopo kupitia Vicoba kwa njia ya mtandao wa Facebook.

 

“Natoa pongezi nyingi kwa IGP Simon Sirro na Polisi Tanzania kwa kuwakamata watu waliokuwa wanatumia vibaya jina langu, la mke wangu Salma na mwanetu Ridhiwani kuwahadaa na kuwaibia Watanzania ninaowapenda sana. Kubainika kwa mtandao huo na kukamatwa ni hatua nzuri ya kupongezwa,” alisema Jakaya Kikwete.

 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa watu hao ambao wamekamatwa na jeshi hilo la polisi watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

 

VIDEO: MSIKIE RPC MAMBOSASA AKIELEZEA TUKIO HILO

The post JK Atoa Kauli kwa Jeshi la Polisi appeared first on Global Publishers.