
KAMPUNI inayotoa ya Mikopo Wezesha Mzawa Microfinance Ltd leo imetoa elimu kuhusu huduma zake za mikopo yenye riba nafuu na haraka. leo imetoa elimu kuhusu huduma zake za mikopo yenye riba nafuu na haraka.
Elimu hiyo ilitolewa leo kwa wauguzi wa Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (MOI) jijijni Dar esSalaam ambapo meneja wa kampuni hiyo, Maimuna Tumba, amesema kuwa kampuni yake inatoa fursa kwa Watanzania binafsi ikiwa ni pamoja na kulipia ada za masomo kwa watoto na wanafunzi.
Alifafanua kwamba mikopo ya kampuni hiyo huchukua muda mfupi zaidi kutolewa kwa ajili ya kulipia ada za ngazi zote kuanzia shule za msingi, sekondari na vyuo mbalimbali kwa riba na masharti nafuu ambayo mkopaji anatakiwa kuwa Mtanzania mwenye umri usiokuwa chini ya miaka 18.
Aliongeza kwamba mkopaji anaweza kuwa mfanyakazi au mfanyabiashara ambaye atawajibika kuleta vielelezo vya shule au chuo husika ili ofisi iweze kuvihakiki na akikidhi vigezo fedha hutalipwa moja kwa moja kwenye shule au taasisi husika.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Wezesha Mzawa Microfinance, Shamimu Mshana, alifafanua kuwa lengo hasa ni kutoa suluhisho la kweli kwa watu wenye mahitaji ya fedha kwa uharaka na muda mfupi.
“Tunatoa kwa mfanyabiashara halali anayezingatia ulipaji kodi katika mamlaka husika na mkopaji anaweza kurudisha kiasi alichokopa kulingana na yeye mwenyewe atakavyoona kwa mujibu wa mahitaji yake, ” alisema.
Naye, mhamasishaji mashuhuri wa ujasiriamali nchini aliyehudhuria hafla hiyo, Eric Shigongo, aliyefika hapo kwa ajili ya kuwatia moyo na kuwapa mbinu za kujikwamua kiuchumi washiriki, alisema kuwa haiwezekani mfanyakazi akawa anasubiri mshahara tu na kwamba ni lazima atengeneze vitegauchumi vingine ili aondokane na umaskini.
Amesema wafanyakazi wengi hutumia kigezo cha kwamba muda wa kutoka kazini ni mrefu na hivyo wanashindwa kufanya majukumu mengine ya kujiongezea kipato.
Pamoja na hivyo, aliwashauri kuondokana na dhana hiyo na wautumie muda huo wa kuanzia jioni kwa kufanya kazi za kuwaongezea vipato kiuchumi.
Aliwashauri waitumie kampuni hiyo ya Wezesha Mzawa Microfinance Ltd ili waongeze mitaji yao na kuendeleza biashara
The post ‘WEZESHA MZAWA’ YATOA ELIMU YA MIKOPO MUHIMBILI KAMPUNI appeared first on Global Publishers.