NEWS

1 Aprili 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 73 na 74 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA-
0657072588
ILIPOISHIA  
Livna aliendelea kuzungumza naneno ambayo yalizidi kukasirisha Mariam ambaye ninatambua kwamba ana nipenda. Taratibu Mariam akapiga hatua mbili mbele  na kuniacha mimi nyuma.
“Mari…..”
Kwa jicho alio nitazama nalo Mariam nilijikuta nikinyamaza kimya, Mariam akaachia msunyo mkalia na kumsogelea Livna sehemu alipo simama.
“Sipambani kwa ajili ya huyu mwanaume, ila ninapambana kwa ajili ya uhuru wangu”
Mariam baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo, akamtandika Livna kichwa kizito cha pua, na kumfanya ainame chini huku akitoa mlio wa maumivu, kitendo kilicho pelekea wasichana wota hawa kuanza kutushambulia kwa hasira kali.

ENDELEA
Nikazidi kujitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha ninawahimili hawa wasichana wenye mafunzo makubwa ya kupambana, kila nilivyo jaribu kadri ya uwezo wangu, nilijikuta nikishindwa kabisa, kipigo ambacho ninakipata mfululizo kikanifanya taratibu kuanza kuishiwa nguvu na kuanguka chini, kwa macho yaliyo jaa ukungu wa damu inayo nimwagika kutoka kwenye baji la uso baada ya kuchanwa na kitu chenye makali, nikamuona jinsi Mariam naye akipokea kipigo kikali hadi akaanguka chini na kuulia kimya. Msichana moja pasipo kuwa na huruma, akanikanyaga kichwani mwangu kwa kiatu chake chenye ncha kali na kujikuta giza jingi likinitawala kwenye mfumo wa kuona, taratibu mawasiliano ya ubongo na mwili yakakatika.
                                                                                                          ***
    Mlio wa mashine ambayo sifahamu ni mashine ya nini, nikaanza kuisikia kwenye masikio yangu. Taratibu nikafumbua macho yangu, ukungu mzito uliopo kwenye macho yangu sikuweza kuona chochote katika chumba hichi, nikazidi kujitahidi kuyafumbua macho yangu, kwa sekunde kadhaa nikaanza kuona baadhi ya vitu ambavyo taratibu nikaanza kuvigundua kwani si mara yangu ya kwanza.
Taa mbili za mwanga mweupe zilizo juu ya chumba hichi, zikanifanya niweze kuyaona mandhari ya chumba hichi ambacho nimegundua ni hospitalini.
Mashine ya kugemea iliyopo pembeni yangu iliyo unganishwa na mtungi wa hewa ya oksijeni, vikazidi kunihakikishia kwamba eneo nililopo ni hospitalini. Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo macho yangu yalivyo weza kuona mandhari ya chumba hichi ambacho sijamuona mtu yoyote.
Nikiwa katika hali ya kufukiria ni kitu gani kilicho pelekea mimi kuwa katika hali hii, mlango wa hichi chumba ukafunguliwa na akaingia nesi wa kike aliye valia mavazi meupe ya kupendeza.

“Karibu duniani”
Nesi huyo alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Nipo wapi?”
“Upo sehemu moja isiyo na jina”
“Isiyo na jina?”
“Yaa ila mimi sio mzungumzaji mkubwa katika hilo, ila yupo ambaye atazungumza”
Nesi huyo akatoka chumba humu, huku kwa mara kadhaa akinitazama kitandani nilivyo laa. Nesi huyu mwenye asili ya kiafrika amenifanya nianze kuwaza mambo mengi sana akilini mwangu, na kitu kingine ambacho kinanichanganya ni yeye kuwa na uwezo wa kuzungumza Kiswahili. Nikaendelea kulala kwenye hichi kitanda huku nikitafakari mambo mengi sana kwenye maisha yangu. Baada ya lisaa moja akaingia mwana mama mrefu aliye valia gauni jeusi pamoja viatu virefu. Ana umbo lililo jengeka vizuri kwa mazoezi huku makalio yake ni makubwa kiasi. Akatembea kwa hatua za taratibu hadi pembeni ya kitanda changu, huku akinitazama usoni mwangu akiwa na tabasamu pana.

“Habari yako kijana”
Mama huyu alizungumza kwa Kiswahili fasaha kabisa hadi mimi mwenyewe nikabaki nimemkodolea macho tu.
“Habari yako kijana?”
“Ahaa salama tu”
“Kwanza nina furaha kukuona ukiwa upo hai”
Mama huyu alizungumza huku  akivuta kiti na kukiweka pembeni ya kitanda, kisha akakaa huku ananitazama usoni.
“Hapa ni wapi?”
“Upo Afrika kusini”
“Afrika kusini!!!!”
Nilijikuta nikishangaa, nikajaribu kukaa kitaki kitandani ila nikajikuta nikiwa nimeshindwa kutokana na maumivu makali ya kichwa.