KUFUATIA matoleo ya simu mbalimbali yaliyotangulia, TECNO, imekua ikitajwa ikihusishwa na ujio wa toleo jipya ikikisiwa kuwa ni muendelezo wa matoleo ya Camon, ni ukweli usiopingika kuwa matoleo ya TECNO-Camon yamekua na kamera nzuri zaidi kufananishwa na matoleo mengine.
Miongoni mwa vivutizi vinavyoipa simu kipaumbele, bila shaka simu inatakiwa iwe na kamera yenye megapixel kubwa, TECNO, wamelizingatia hilo.
Baadhi ya kurasa za mitandaoni zimeihusisha kampuni ya TECNO juu ya ujio wa toleo jipya likipewa jina la Camon kufuatia histoia ya kampuni kuzindua Camon CX mwaka jana miezi kama hii, bado hakujawa na uhakika wa taaifa hizi hivyo ni propaganda tu.
Simu hiyo inakadiriwa kuwa na megapixel 16 mbele pamoja na flashi maalum kwa picha za ‘’selfie’’, uwezo wa kupiga picha zenye ubora wa HD, kamera yake ya nyuma kuja na megapixel nyingi zaidi sambamba na flashi maalum zinaakisi mwanga ili kupata kuendana na mazingira.
Maswali kuhusiana na ujio wa simu hiyo `yamekua mengi sana pasina kupata majibu yenye uhakika, kamera inayoweza kupiga picha nyingi ndani ya mda mfupi zikiwa na ubora wa HD, bado inaacha maswali yanayoamsha morali ya kutaka kujua zaidi.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti http//www.tecno-mobile.com
The post TECNO KUJA NA KAMERA YA AINA YAKE appeared first on Global Publishers.