NEWS

12 Juni 2018

UKWELI KUHUSU WANAFUNZI UDSM WALIOFARIKI DUNIA AJALINI USIKU

KUFUATIA taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu mwanafunzi Maria Godian Soko aliyefariki dunia kwa ajali usiku wa kuamkia leo maeneo ya Ubungo Riverside, Dar es Salaam ikisemekana kuwa alikuwa mjamzito, Katibu Mteule wa Serikali ya Wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Hussein Amri Aman, amekanusha taarifa hizo na kusema zinapaswa kupuuzwa.

 

Amri amesema kwamba marehemu Soko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya pumu kwa muda mrefu halim iliyokuwa ikisababisha apoteze fahamu, ndiyo sababu kuu iliyomfanya awe anakimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa (ambulance).

 

Marehemu Maria alikuwa na matatizo ya pumu ambayo yalimsababishia kifua kubana hadi kuzimia, majira ya saa mbili kasoro usiku tulifanya utaratibu wa kuita ambulance ya chuo na kumchukua hapa mabibo hostel kumpeleka hospitali ya chuo kwa matibabu zaidi”

 

Ameongeza “Wakati taratibu za kumpeleka hospitali ya chuo zinaendelea ndipo ajali mbaya ikatokea pale riverside, taarifa zinazoendelea kusambaa kwamba marehemu alikuwa mjamzito anaenda kujifungua sio za kweli”.

 

Katika ajali hiyohadi sasa walioripotiwa kufariki ni wanafunzi wawili ambao ni Maria Godian Soko (Mwaka wa kwanza COSS) na Steven E Sango  (CPE CoET mwaka wa pili) pamoja na dereva James.

 

Mwanafunzi mwingine aliyekuwepo katika msafara huo ni Abishai Nkiko (Bsc Industrial Engineering mwaka wa 3 CoET) hali yake ni mbaya na anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili.

 

Maria Godian Soko ( B.A in psychology mwaka wa kwanza) amefariki jana usiku baada ya ambulance ya chuo kugongana na lori majira ya saa mbili  maeneo ya riverside -Ubungo  wakati alipokuwa akikimbizwa hospitali  baada ya kubanwa na pumu hali iliyomfanya kupoteza fahamu.

The post UKWELI KUHUSU WANAFUNZI UDSM WALIOFARIKI DUNIA AJALINI USIKU appeared first on Global Publishers.