Kesi inayowakabili vigogo tisa wa Chadema, wakiongozwa na mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe inaendelea muda huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Waziri Mkuu wa Mstaafu, Edward Lowassa ametinga katika mahakama hiyo, akiambatana na viongozi wa chama, akiwemo Mbowe.
Wengine walioingia mahakamani hapo ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu John Mnyika (Bara), Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu (Zanzibar) na mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.
Mahakama leo kupitia Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri inatarajiwa kutoa uamuzi kama upande wa utetezi (wakina Mbowe) ukate rufaa ama lah
