NEWS

12 Juni 2018

Zari Athibitisha Kuwa Hajarudiana na Diamond

Zari The Bosslady

MPENZI wa mwanamuziki Diamond Platnumz kwenye ngoma ya Iyena, Zari The Bosslady amethibitisha taarifa kuwa yeye na Diamond hawajarudiana bali wameelewana kwa ajili ya kulea watoto wao.

 

Tangu wiki iliyopita kulikuwa na tetesi zilizodai kuwa Diamond na Zari wamerudiana baada ya wawili hao kuonekana pamoja nchini South Africa na watoto wao.

Diamond Platnumz akifanya yake kwenye ngoma ya Iyena na Zari The Bosslady.

Zari amefungukia tetesi hizo na kusema yeye na Diamond hawajarudiana kuwa wapenzi bali wameamua kuelewana kwa ajili ya kulea watoto wao.

Zari amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Snapchat ambapo aliandika:
Tetesi za Diamond na Zari kurudiana zilianza baada ya wawili hao kukutana nchini South Africa baada ya kutoanana kwa miezi minne baada ya kuachana.

The post Zari Athibitisha Kuwa Hajarudiana na Diamond appeared first on Global Publishers.