Marehemu Bi. Monica Joseph Magufuli enzi za uhai wake.
Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Rais Magufuli jana alifika katika Chumba cha uangalizi Maalum ICU katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza kumjulia hali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipomtembelea kumjulia hali Dada yake Monica Joseph Magufuli s jana ambapo alikuwa amelazwa katika Chumba cha uangalizi Maalum ICU katika hospitali ya Bugando mkoani Mwanza.
NASIKITIKA kuwajulisha kuwa Dada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Monica Joseph Magufuli amefariki dunia asubuhi leo tarehe 19 Agosti, 2018 katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza. Natoa pole kwa Mhe. Rais Dkt. J.P Magufuli, Familia na wote walioguswa na msiba huu pic.twitter.com/q5FwQk3kdj
— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) August 19, 2018
The post Breaking News: Rais Magufuli Afiwa na Dada Yake appeared first on Global Publishers.