Enzi za wanafamilia waliofariki wakati wa uhai wao.
FAMILIA ya watu watatu na watu wengine zaidi ya 35 wamefariki jijini Genoa, Italia, baada ya daraja kuvunjika.
Roberto Robbiano, mkewe Ersilia Piccinino, na mtoto wao mwenye umri wa miaka saba, Samuel, wamekufa baada ya gari lao kuanguka umbali mrefu kutoka juu katika daraja la Morandi lililojengwa miaka 50 iliyopita.
Ajali hiyo ilitokea mchana saa 5:30 jana (Jumanne) ambapo watu wengi waliangukiwa mabaki ya zege na takataka zingine na ikabidi kutafutwa kwa muda mrefu wakiwa tayari wamekufa.
Taswira za ajali hiyo na sehemu zilizosababisha daraja kuvunjika (picha ya chini).
The post FAMILIA YA WATATU, 35 WAFARIKI AJALI YA DARAJA KUVUNJIKA appeared first on Global Publishers.