Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Barnabas Mwakalukwa, amekanusha kwamba, hakuna mtuhumiwa anayelazimishwa kutoa dhamana ya pesa kama inavyodaiwa na baadhi ya raia pindi wanapotakiwa kufanya hivyo.
Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa BreakFast kinachorushwa na East Africa Radio, Mwakalukwa amesema, dhamana inayotolewa polisi huwa ni ya maandishi lakini kumekuwa na watu wa daraja la kati wanaowalaghai watu kuwa watoe pesa ili wasaidiwe kutoka chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.
''Ukitoa rushwa ili ndugu yako atoke polisi wewe ndio unakuwa na tatizo, kwanini utoe rushwa wakati ukifuata utaratibu ndugu yako atapata dhamana tu kama kosa lake linaruhusu'', amehoji Mwakalukwa.
Aidha, amefafanua kuwa, 'Mahabusu sio nyumba ya kuishi hivyo mtuhumiwa akienda atahojiwa kwa muda na huenda akarudi mtaani na ni utaratibu wa kawaida na si kweli kwamba wanatoa rushwa ili watoke mahabusu.
Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), polisi katika mikoa ya Iringa na Temeke wamenyooshewa kidole kwa kuongoza kwa vitendo vya kuomba na kupokea rushwa.