NEWS

16 Agosti 2018

MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI

Mhe Jaji Makaramba akisaini kitabu cha wageni.

Mhe. Dkt. Levira akisoma taarifa ya makabidhiano ya ofisi

Hafla hiyo ikiendelea.

Watumishi wakimsikiliza Mhe. Makaramba (hayupo pichani).

Jaji Mfawidhi-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi na baadhi ya Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya, (wa tatu kushoto) ni Mhe. Jaji Paul Joel Ngwembe, (wa pili kulia) ni Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira, wa kwanza kulia ni Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya,  Mhe. George Herbert, wa pili kushoto ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. William Mutaki na wa kwanza kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Bw. Moses Mwidete.

Mhe Makaramba akipanda mti wa kumbukumbu.

Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira akianda mti.

Mhe Ngwembe akipanda mti wa kumbukumbu.

Watumishi wa Mahakama Kanda ya Mbeya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano bila kujali vyeo na kufanya kazi kama timu moja, kupendana na kufuata C tatu yaani ‘Coordination, Cooperation na Consultation’  ili kuwahudumia wananchi ipasavyo

.

Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi mpya wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya, Mhe. Robert Makaramba alipokuwa akiongea na Watumishi wa Kanda hiyo baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi  Agosti, 15 2018, katika ofisi za Mahakama Kuu mkoani Mbeya.

 

Mhe. Jaji Makaramba alisisitiza viongozi wa ngazi ya juu ya Kanda hiyo yaani Jaji Mfawidhi, Naibu Msajili na Mtendaji wa Mahakama kufanya kazi kwa kufuata kile alichokiita utatu mtakatifu’

 

 Aidha, pamoja na mambo mengine, Mhe. Makaramba alisisitiza juu ya nidhamu na uadilifu wa watumishi wa Mahakama huku akikemea Watumishi kutojihusisha na vitendo vya rushwa ili kwa pamoja kuweza kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa miaka mitano (2015-2020) wa Mahakama.

 

“Mtumishi akikamatwa kwa tuhuma za rushwa nitamsindikiza mwenyewe hadi TAKUKURU nikifika nawakabidhi wamalizane naye wenyewe” alisema Jaji Mfawidhi huyo.

 

 

Mhe. Makaramba vilevile  aliupongeza uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa kazi nzuri ya ukarabati wa jengo la Mahakama Kuu Mbeya ambalo pia hutumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi pamoja na Mahakama ya Wilaya Mbeya na kuwataka Watumishi kulitunza vyema jengo hilo pamoja na vitendea kazi vya kisasa vilivyomo.

 

 

Aidha; Mhe. Jaji Makaramba alitoa maagizo ya kuwa na mpango kazi wa Kanda ambao utaenda sambamba na mpango Mkakati wa Mahakama kitaifa ili kutengeneza mazingira mazuri  na wezeshi ya kuwahudumia wananchi.

 

 

Aliongeza kwa kusema kwamba yupo tayari kutoa mchango wake kadri akatavyojaaliwa na Mwenyezi Mungu vile vile ataendelea kujifunza kutoka kwa watumishi wa Kanda ya Mbeya mambo mbalimbali yatakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa wakati.

 

 

Viongozi na Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya wamempokea Mhe Robert Makaramba ambaye amehamishiwa mkoani humo kuwa Jaji Mfawidhi wa Kanda hiyo kujaza nafasi ya Jaji Mfawidhi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwepo kustaafu kwa mujibu wa sheria.

 

Pamoja na mapokezi hayo, makabidhiano ya ofisi yalifanyika kati ya Mhe. Makaramba na Mhe. Dkt. Mary Caroline Levira akimwakilisha Mhe. Kaimu Jaji mfawidhi ambaye alipatwa na udhuru.

 

 

Katika hafla hiyo Mhe. Dkt. Levira alisoma taarifa ya makabidhiano ya ofisi ikijumuisha mambo muhimu ikiwepo eneo la utawala wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kwa kueleza kuwa Kanda ya Mbeya inajumuisha Mikoa ya Mbeya na Songwe.

 

Vilevile katika taarifa hiyo kulikuwa na taarifa ya hali ya mashauri, hali ya watumishi, hali ya miundombinu, hali ya fedha na  hali ya vyombo vya usafiri.

 

Na Rajabu Singana, Mahakama Kuu Mbeya

The post MAHAKAMA KUU KANDA MBEYA YAPATA JAJI MFAWIDHI appeared first on Global Publishers.