NEWS

24 Agosti 2018

MAONI YAPOKELEWA KUIFANYA DODOMA KUWA MAKAO MAKUU

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeanza kupokea maoni ya wadau mbalimbali kuhusu muswada wa tamko la kulifanya Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi kwa mujibu wa kanunu za kudumu za Bunge.

 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jasson Rweikiza amesema lengo la kukusanya maoni yao ni kuwezesha kuwepo kwa muswada ambao utatungiwa sheria ambayo italinda tamko hilo baadae lisije kubadilishwa.

 

Miongoni mwa wadau waliokutana na kamati hiyo ni Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma Profesa Davies mwamfupe ambaye anasema endapo sheria ya kuitambua Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi itarahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya mikoa na mikoa na nchi jirani kutokana na jiografia yake.

 

Kamati hiyo kwa kuanza imekutana na taasisi kumi wakiwemo wawakilishi kutoka  jiji la dodoma na chuo cha serikali za mitaa hombolo.

The post MAONI YAPOKELEWA KUIFANYA DODOMA KUWA MAKAO MAKUU appeared first on Global Publishers.