NEWS

23 Agosti 2018

MBOWE: Waliomuua Akwilina Wapo, Mnataka Kutufunga, Hatuogopi – Video

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa, Freeman Mbowe, amezungumza na waandishi wa habari leo Agosti 23 na kufafanua kwa kina kuhusu kinachoendelea juu ya kesi inayomkabili na viongozi wenzake nane ambayo inasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

 

Katika mazungumzo yake Mbowe pamoja na Chadema kwa ujumla wameonesha kutokuwa na imani na Hakimu anayesimamia kesi yao anayeitwa, Wilbard Mashauri kwa kile wanachodai kuwa anafanya kazi kwa maelekezo kutoka sehemu yaliyolenga kuwafunga na kutowatendea haki.

The post MBOWE: Waliomuua Akwilina Wapo, Mnataka Kutufunga, Hatuogopi – Video appeared first on Global Publishers.