NEWS

16 Agosti 2018

NEC: Ubalozi wa Marekani Wametoa Tathmini Wakiwa Kama Nani? – Video

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema imeshangazwa na taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, jana Agosti 8, 2018 kwamba uchaguzi mdogo wa Buyungu na Arusha ulikuwa si wa huru na haki.

 

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam na kusema kwamba wao kama Tume, kwa mujibu wa sheria walitoa nafasi kwa taasisi kuomba kuwa waangalizi wa ndani wa uchaguzi huo, lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza kuomba, hivyo jambo la Ubalozi wa Marekani kutoa tathmini hiyo ilihali hawakuhusika kuangalia uchaguzi ni mshangao mkubwa kwa NEC.

 

“Chaguzi zetu zote zinaongozwa kwa katiba ya nchi, sheria, kanuni na desturi za uchaguzi. NEC tulikaribisha waangalizi wa ndani, lakini hakuna hata mmoja aliyejitokeza, kwa balozi zetu hapa nchini nazo zilikuwa na fursa ya kuleta maombi yao kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, lakini hatuna taarifa ya ubalozi wowote katika nchi hii iliyofata taratibu za kisheria kutaka kufanya uangalizi.

 

“Tunashindwa kufahamu iwapo tamko hili limetolewa na ubalozi huu (Marekani) kama mshiriki kufanya uangalizi wa uchaguzi, au umetoka wapi? Kumbukumbu zetu hazionyeshi kama taratibu zetu ziilifuatwa na kurushu Ubalozi wa Marekani kufanya uangalizi huo,” amesema jaji Kaijage.

 

Aidha, Kaijage amesema wagombea waliokuwa na amalalamiko yao waliyawasilisha NEC na yalishughulikiwa kwa mujibu wa sgheria wala hakuna hata rufaa moja iliyoshindwa kusikilizwa.

 

VIDEO: MSIKIE JAJI KAIJAGE AKIFUNGUKA

The post NEC: Ubalozi wa Marekani Wametoa Tathmini Wakiwa Kama Nani? – Video appeared first on Global Publishers.