NEWS

18 Agosti 2018

NMB Waziundua Huduma ya Kufungua Akaunti Kupitia Simu yako Mkononi

Benki ya NMB mapema wiki hii walifanya uzinduzi wa huduma tatu mpya za Benki hiyo uliofanyika Hotel ya Hyatt na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha, teknolojia na baadhi ya wateja wa NMB. 

Huduma zilizozinduliwa ni uwezo wa mwananchi kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi, App yenye huduma zote ambazo mteja anaweza kufanya mwenyewe badala ya kwenda kwenye tawi na Scan to Pay huduma ya kufanya malipo kwa kutumia QR code na hivyo kuwawezesha kulishikishwa kifedha. 

App ya NMB KLiK inapatikana katika Playstore https://goo.gl/Fr9fZf na kupitia AppStore https://goo.gl/wQXZV6

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk.Benard Kibese ambaye alisema kwamba ubunifu huo utarahisha Watanzania wengi kufungua akaunti za benki hiyo kupitia simu zao za mikononi na kwamba hivi sasa watumiaji wa simu za mkononi ni wengi na hivyo huduma hiyo ya NMB imekuja wakati sahihi. 

“Tunaipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao wa kuhakikisha wanatumia teknolojia iliyopo kuanzisha huduma za kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi na kizuri zaidi hata wenye simu za tochi bado wanaweza kufungua akaunti kupitia huduma hiyo,” alisema Dk.Kibese.

Huduma hii imepokelewa vizuri na watumiaji wa mtandao wa Twitter ambao wamesema kwamba uzinduzi huo ni muhimu sana hususani katika mchakato wa kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa kati.