NEWS

16 Agosti 2018

RAMBO: MABONDIA MAYWEATHER, PACQUIAO WATARUDIANA

                          Rambo.

MWIGIZAJI Sylvester Stallone (Rambo) wa Marekani, amesema bondia Floyd Mayweather wa Marekani atakubali wito wa mpinzani wake,  Manny Pacquiao wa Ufilipino wa kurudiana katika muda mfupi ujao,  kuzichapa ndondi.

“Nina uhakika wa asilimia 99 kwamba hilo litatokea,” alisema Rambo akiwa katika sherehe ya kuzaliwa kwa mkewe,  Jennifer Flavin huko Spago.

“Wana kila sababu ya kurudiana, ikiwemo kutunza heshima, fedha, historia na vingine vingi,” alisisitiza na kuelezea kauli ya Pacquiao aliyoitoa mwezi Julai mwaka huu baada ya kumshinda Lucas Matthysse,   hivyo akataka warudiane ne Floyd.

Mayweather,  Pacquiao wakizipiga.

 

The post RAMBO: MABONDIA MAYWEATHER, PACQUIAO WATARUDIANA appeared first on Global Publishers.