NEWS

15 Agosti 2018

SAFAREE: MINAJ ALINICHOMA KISU AKITAKA KUNIUA

MWANAMUZIKI wa Marekani na Jamaica, Safaree amedai kwamba msanii na mwanamitindo wa Marekani,  Nicki Minaj,  alimchoma kisu sehemu kubwa na kusababishwa akimbizwe hospitali.

Hata hivyo, Minaji amsema huo ni uwongo.

Safaree, aliyeachana na Nicki mwaka 2014, alituma ujumbe kwenye mtandao kwamba: “Kumbuka usiku ulionikata kisu na polisi wananibeba kwenye gari la wagonjwa katika machela nikadanganya kwamba nilitaka kujiua ili usikamtwe na kufungwa.”

Nicki naye alijibu: “Uliiba kadi yangu ya benki ukifikiri utapata fedha ya bure. Mungu atakuadhibu kwa kudanganya.”

Hata hivyo, TMZ limesema liliwahi kuona video mwaka 2014 ikimwonyesha Nicki akimfukuza Safaree akiwa na kisu.

The post SAFAREE: MINAJ ALINICHOMA KISU AKITAKA KUNIUA appeared first on Global Publishers.