NEWS

16 Agosti 2018

Steve Nyerere Afunguka Skendo ya Kuchikichia na Rambi Rambi...Adai Hata Acha Kusimamia Misiba

MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, ameibuka na kufungukia skendo ya kuandaa misiba kisha kuchafuka kwa madai kuwa amechikichia rambirambi.

Akizungumza na Amani juzikati mara baada ya kujitoa kuratibu msiba wa mchekeshaji Amri Athuman ‘King Majuto’, Steve alisema suala hilo halimuumizi kichwa kwa sababu kutoka ndani ya nafsi yake anaamini kwamba hachakachui fedha, na anamshukuru Mungu kwamba hivi karibuni wasanii wenzake wamemtia moyo kwamba asiache.

“Angalia wasanii wenzangu wengi sasa hivi wameonesha kuniunga mkono hivyo sitaacha kusaidia pindi misiba inapotokea kwani wamenitia moyo kwamba ninastahili kuwaunganisha katika matatizo,” alisema Steve.

Stori: Memorise Richard