NEWS

15 Agosti 2018

TCDC YAELEZEA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UZAZI WA MPANGO DUNIANI

Meneja wa Utekelezaji wa Miradi wa Asasi ya Tanzania Communication and Development Center (TCDC) James Mlali, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani).

 

KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Uzazi wa Mpango Duniani, Meneja wa Utekelezaji wa Miradi wa Asasi ya Tanzania Communication and Development Centre (TCDC) James Mlali, amesema shughuli mbalimbali zinatarajiwa kufanyika siku hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya njia mbalimbali za uzazi wa mpango.

 

 

Katika siku hiyo ambayo huadhimishwa Septemba 26, duniani kote, huduma na vifaa vinavyotumika katika uzazi wa mpango, vitaoneshwa na elimu kutolewa kwa wananchi wote, huku pia wadau wakijadiliana jinsi jumuiya za kimataifa zinavyotekeleza mikakati ya uzazi wa mpango.

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mlali amesema uzazi wa mpango huwawezesha akina mama na wasichana katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kuleta uwiano sawa katika makundi ya kiuzalishaji na kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na hata kuwa na nafasi ya kujiendeleza kwenye shughuli mbalimbali kama vile za kielimu.

 

 

The post TCDC YAELEZEA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA UZAZI WA MPANGO DUNIANI appeared first on Global Publishers.