Ni vigumu sana kutofautisha kati ya madeni ya ukoo na vifungo vya ukoo lakini katika makala haya nitaelezea tofauti kati ya madeni ya ukoo na vifungo vya ukoo.
MADENI YA UKOO NI NINI ?
Madeni ya ukoo ni mapigo ambayo huwapata watu wa ukoo fulani kwa sababu mababu wa ukoo huo walivunja maagano waliyo ingia na mizimu au miungu wa ukoo.
Mababu wa ukoo walipoingia katika maagano na mizimu wa ukoo walipewa masharti ambayo walitakiwa kuyafuata na miiko ambayo hawakutakiwa kuivunja.
Lakini baada ya kuvunja maagano hayo mizimu wa ukoo huo waliachilia mapigo kwa watoto wa mababu hao pamoja na vizazi vyao vyote.
Haya ni mapigo ambayo kila mtoto anaezaliwa katika ukoo huo ni lazima ayapate. Mapigo hayo yanaweza kuwa maradhi kama vile pumu, kifafa, kisukari nakadhalika.
Yanaweza kuwa vijana wa ukoo Fulani kufa mapema nakadhalika nakadhalika.
Mbali na kuvunja maagano ya ukoo, madeni ya ukoo pia yanaweza kusababishwa na maapizo yaliyo fanywa na mwanaukoo dhidi ya ukoo.
Kwa mfano kuna kisa kimoja maarufu kuhusu ukoo mmoja unao toka katika mkoa mmoja uliopo hapa hapa nchini Tanzania.
Mababu wa ukoo huo walikuwa na dada yao mmoja ambae alikuwa mgumba.
Dada yao huyo alinyanyaswa sana na wana ukoo kwa sababu ya hali yake ya ugumba.
Manyanyaso yalipo mzidi alienda hadi kwenye eneo yalipo makao makuu ya mzimu wa ukoo huo na kujiapiza kwa uchungu mkubwa sana kwamba “ KWA VILE WANA UKOO HUO WAMEMTENGA NA KUMNYANYASA KWA SABABU YA YEYE KUWA MGUMBA, BASI HAKUNA MTOTO YOYOTE WA KIKE ATAKAE ZALIWA KATIKA UKOO HUO AMBAE ATAKUJA KUBEBA UJAUZITO AU KUZAA MTOTO”
Alivyo maliza kufanya maapizo hayo mwanamke huyo alijitoa yeye mwenyewe kama kafara kwa ajili ya kusimamisha maapizo yake.
Basi mzimu wa mwanamke huyo uliwatesa wana ukoo huo kwa muda mrefu sana.
Kila mwanamke aliekuwa anazliwa katika ukoo alikuwa hapati ujauzito.
Ilifikia kipindi ambacho endapo mtoto wa kike aliEzaliwa katika ukoo huo atabeba ujauzito basi hiyo ilichukuliwa na wazee kama ishara kwamba mtoto huyo wa kike sio mtoto wa ukoo huo yani hajazaliwa na mwanaume kutoka kwenye ukoo huo.
VIFUNGO VYA UKOO
Vifungo vya ukoo ni mambo ambayo watu kutoka katika ukoo Fulani hutakiwa kuyafanya au hawaruhusiwi kuyafanya kwa sababu ya maagano ya kiroho yaliyo ingiwa na mababu wa ukoo huo kwa ajili ya ukoo.
Maagano haya huwajumuisha na kuwafunga wana ukoo wote kuanzia walio kuwa hai wakati maagano yanaingiwa hadi watakao kuja kuzaliwa katika vizazi na vizazi.
Maagano hayo huendana na masharti maalumu ambayo ili agano liendelee kusimama basi watu wa ukoo huo ni lazima wayatimize.
Masharti haya ndio ambayo hujulikana kama miiko.
Kila mtu anaezaliwa katika ukoo huo hutakiwa kutunza na kuheshimu miiko hiyo na endapo ataenda kinyume basi atapata adhabu ambayo iliwekwa wakati maagano yanaingiwa.
Mfano kuna baadhi ya koo kwao ni mwiko kutoa mimba . Mwanamke yoyote yule aliezaliwa katika koo hizo haruhusiwi kutoa ujauzito hata wa wiki moja na mwanamke yoyote yule ambae atabeba ujauzito wa mwanaume ambae anatoka katika ukoo huo pia haruhusiwi kutoa ujauzito.
Mwanamke yoyote kutoka katika ukoo huo ambae atathubutu kutoa mimba basi atakufa .
Na mwanamke yoyote atakae toa ujauzito wa mwanaume anae toka katika ukoo huo atakufa endapo atajaribu kutoa ujauzito huo.
Hijalishi unafahamu ama haufahamu kuhusu muiko huu endapo utaukiuka basi utakufa ilimradi tu upo katika ukoo huo.
Kwa ufupi tofauti kubwa kati ya madeni ya ukoo na vifungo vya ukoo ni kwamba madeni ya ukoo haya ni mapigo ambayo kila mtu anaezaliwa ndani ya ukoo Fulani ni lazima ayapate kama malipo ya kisasi cha mizimu wa ukoo dhidi ya wana ukoo huo kwa sababu ya maagano ambayo mababu wa ukoo huo waliyaingia na mizimu hao na kuyavunja.
Lakini vifungo vya ukoo ni miiko ambayo kila mwana ukoo wa ukoo Fulani anatakiwa kuifuata na endapo asipo ifuata au endapo ataivunja basi atapata mapigo Fulani.
Mtu anaweza kujiepusha na vifungo vya ukoo kwa kufuata miiko ya ukoo wake na kutoivunja lakini madeni ya ukoo hawezi kujiepusha nayo kwa sababu tayari mababu zake walikwisha fanya makosa hivyo analipia madeni ama makosa ya babu zake.
Mtu anaweza kujiepusha na madeni ya ukoo kwa kuvunja maagano ambayo babu zake waliingia na mizimu wa ukoo.
VIPI KUHUSU MADENI YA FAMILIA ?
Kama ilivyo kwa koo, familia nazo huwa na madeni ingawa madeni ya familia huwa tofauti kidogo na madeni ya ukoo.
Tofauti yake ni moja ni kwamba madeni haya ya wanafamilia huwa gusa watu wa familia peke yake. Hayavuki nje ya familia.
Mwanafamilia hii anaweza kuwa na madeni ya ukoo lakini wakati huo huo anakuwa na madeni ya familia ambayo yanamuhusu yeye na wanafamilia wenzake lakini hayawahusu wana ukoo wake.
Mfano. A na B ni mtu na kaka ake. A na B wanatoka UKOO C ambao una madeni ya ukoo au vifungo vya ukoo ambavyo A na B wanatakiwa kuvilipa.
Wakati huo huo A ana familia yenye mke na watoto watano. A ana madeni ya familia . Madeni ya A hayamuhusu B hata kidogo wala watoto wa B ila yanamuhusu A na watoto wa A.
MADENI YA FAMILIA NI NINI ?
Madeni ya familia ni mapigo ambayo huwaandama na kuwapata watu kutoka familia Fulani kwa sababu ya makosa yaliyo fanywa na wana familia hao eidha wote kwa pamoja au asilimia kubwa ya wanafamilia hiyo au viongozi wa familia hiyo.
Mfano : Kuna pigo moja ambalo huwaandama sana wanawake wanao toka katika familia za watu wenye uwezo .
Pigo hili lina husiana na WADADA WA KAZI ZA NYUMBANI ama MAHAUSIGELI.
Familia inayo wanyanyasa wadada wa kazi ijue inapanda mbegu mbaya sana ya kiroho kwa watoto wa kike kutoka katika familia hiyo.
Watoto wa kike kutoka katika familia zinazo watesa na kuwanyanyasa mahausigeli huwa WANANYANYASWA SANA KATIKA NDOA ZAO.
Haijalishi wadada hao walishiriki au hawakushiriki katika kuwatesa na kuwanyanyasa mahausigeli hao lakini wanapo ingia kwenye ndoa zao huwa WANATESWA NA KUNYANYASIKA SANA.
Nikiwa kama tabibu wa tiba za jadi nimekutana na kesi kama hii nyingi sana. Kama wewe una mdada wa kazi nyumbani kwako. Basi jitahidi kuishi nae vizuri. Usimtese wala kumnyanyasa kwani kwa kumfanya hivyo unakuwa umekopa deni ambalo malipo yake atakuja kuyalipa mtoto wako kwa mume wake pindi atakapo kuja kuolewa.
Mfano mwingine wa madeni ya familia ni pale mama anapo muondoa baba ili aweze kurithi mali.
Hili ni kosa kubwa sana katika ulimwengu wa rohoni.
Watoto wa kike walio zaliwa katika familia hii huwa hawaolewi kabisa na ikitokea wameolewa basi ndoa huvunjika ndani ya muda mfupi sana.
Mwanamke anapomtoa mumewe ili arithi mali maana yake katika ulimwengu wa rohoni ni kwamba familia hiyo haihitaji mume.
Wao wanachohitaji ni mali tu . Hakuna mume atakae ingia ndani ya familia hiyo. Kama pesa wanaweza kupata pesa nyingi sana, kama mali wanaweza kupata mali nyingi sana lakini waume hawawezi kupata kwa sababu waume hawatakiwi katika nyumba hiyo.
Hiyo ni mifano michache lakini ipo mifano mingi sana. Tugusie kidogo kwenye madeni ya nafsi.
VIPI KUHUSU MADENI NAFSI ?
Haya ni mapigo anayo yapata mtu kutokana na mambo mabaya ambayo ameyafanya yeye mwenyewe, maneno ambayo amejitamkia yeye mwenyewe , jina alilo jiita yeye mwenyewe au jina aliloitwa na wazazi wake.
Mambo mabaya ambayo mtu anakuwa ameyafanya yeye mwenyewe ni pamoja na kuwadhulumu yatima na wajane, kuwafanyia dhihaka walemavu, kuvunja agano ambalo ameliingia yeye mwenyewe nakadhalika.
Maneno ambayo amejitamkia yeye mwenyewe ni maneno yote ambayo mtu anakuwa amejitamkia yeye mwenyewe kwa mfano. Kuna watu huwa wanajitamkiaga maneno mabaya wao wenyewe na mwisho wake maneno hayo hugeuka kuwa madeni ambayo hutakiwa kuyalipa.
Kwa mfano mwanamke yupo kwenye ndoa , halafu baada ya kutokea kutokuelewana kidogo na mume wake unamsikia akisema “ Hii ndoa hii, ipo siku ntaondoka tu hapa. Yaani we ngoja tu ipo siku nitaodoka “ Mwisho wa siku mwanamke huyo huondoka katika nyumba hiyo ila hata sababu yoyote ya msingi.
Mfano mwingine unakuta mtu anasema “ Ukitaka kufa mapema wewe tembea na mke wa mtu tu “ halafu baada ya muda Fulani anaingia katika mahusiano na mke wa mtu.
Hilo ni deni la rohoni ambalo lazima alilipe. Mtu huyo kweli atakufa kama alivyo kiri mwenyewe.
Deni la jina alilo jipa mwenyewe au jina alilo pewa na wazazi wake. Jina la mtu ni tamko rasmi kuhusu maisha ya mtu huyo, Ukimuita mtoto wako jina BARAKA maana yake ni kwamba umemtamkia na kumnenea Baraka katika maisha yake. Lakini ukimuita jina mateso, msumbuko, au matatizo jua hilo ni deni tayari ambalo lazima alilipe katika maisha yake.
Kuwa makini sana unapo mpa mtoto wako jina.
VIPI KUHUSU MADENI YA MAENEO.
Kila kijiji kila mtaa kila mji au eneo vinaongozwa na kutawaliwa na roho maalumu. Vijiji na miji ilipokuwa inaanzishwa wazee walifanya matambiko maalumu kwa ajili ya kuingia maagano maalumu na viumbe wa kiroho kwa ajili ya kuutawala na kuulinda mji huo.
Unapo enda kutafuta maisha katika mji Fulani kitu cha kwanza unacho takiwa kujua ni roho zinazo tawala mji huo ili uweze kuendana nazo.
Kuna maeneo mengine yana madeni ya kiroho ambayo kila mtu anaeishi katika eneo hilo ni lazima ayalipe.
Ndio maana unaweza kuta maeneo mengine kijiji kizima au mtaa mzima au kata nzima hakunaga mtu alie fanikiwa au hakuna mtu aliyesoma. Wote wanaishi maisha yanayo fanana na kila anae jaribu kuinuka anashushwa.
Ukienda kuanza maisha katika mji Fulani kitu cha kwanza kabisa unachotakiwa kukijua ni roho zinazo tawala katika mji huo. Hii itakusaidia kujua ni kwa namna gani utaweza kufanya biashara au kutafuta maisha katika eneo hilo.
Ukiona hauwezi kufanya hivyo basi chukua ushauri huu. Badilisha jina la eneo hilo. Jina hilo uwe unalijua wewe mwenyewe na libebe maono yako. Kwa mfano unataka kwenda kuishi katika eneo ambalo watu katika eneo hilo huwa hawafanikiwi, au watoto wote wa kiume wanakuwa mateja na wakike wakuwa machangudoa au wafanyabiashara hawafanikiwi. Wewe ukifika hapo kwa mara ya kwanza tamka rasmi kubadilisha jina la mahali hapo na kuliita jina ambalo linaendana na kile unacho kitaka katika maisha yako au kile ambacho umeenda kukitafuta.
MWISHO KABISA NI KUHUSU MADENI YA SIKU : Haya ni madeni ambayo husababishwa na wachawi na hukusudiwa kulipwa na wakaazi wa kila kijiji na kila mtaa.
Kila siku wachawi wakiwa wanawanga usiku kabla hakujakucha huwa wanamwaga dawa kwenye njia panda zinazo ingia katika mitaa na vijiji mbalimbali na kutamka maneno mabaya dhidi ya wakaazi wote wa eneo hilo.
Maneno hayo ni kama vile : WATU WANAO ISHI KATIKA ENEO HILI WAKIENDA KUFANYA BIASHARA WASIUZE, WANAO TUMIA VYOMBO VYA MOTO WAPATE AJALI, WALIOPO MAOFISINI WAPATE MATATIZO OFISINI, WALIOPO KATIKA NDOA WAPATE MATATIZO KATIKA NDOA ..NAKADHALIKA NAKADHALIKA.
Mambo haya hufanywa kila siku kwa usirias mkubwa sana. Yani wachawi wanapo kuwa wanawangia watu hufanya hivyo kana kwamba maisha yao yanategemea uwanga huo.
Unashauriwa kuwa makini sana.
MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA MUNGWA KABILI. ANAPATIKANA KWA SIMU NAMBA 0744 000 473.
Unaweza kupata maarifa Zaidi kwa kusoma makala zifuatazo:
1. SABABU ZA KIROHO KWA NINI WANAWAKE WAZURI KUPITA KIASI HUWA HAWAOLEWI…………………SEHEMU YA KWANZA.
https://ift.tt/2BuvsCL
2. SABABU ZA KIROHO KWA NINI WANAWAKE WAZURI KUPITA KIASI HUWA HAWAOLEWI…………………SEHEMU YA PILI
3. JINSI WANAWAKE WAZURI KUPITA KIASI WANAVYO IBIWA NYOTA ZAO NA WANAWAKE WENYE UZURI WA KAWAIDA.