NEWS

23 Agosti 2018

Wanaharakati Kenya Waungana Kumpinga Rais Museven wa Uganda


Nchini Kenya wanaharakati pamoja na wanasiasa wamejiunga na wenzao wa Uganda kushinikiza utawala wa rais wa Yoweri Museveni kuzingatia sheria na kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa. Makundi ya kutetea haki za binadamu yamesema yatawasilisha kesi katika mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuishinikiza serikali ya rais Museveni kuzingatia sheria dhidi ya wafungwa wa kisiasa.