NEWS

15 Agosti 2018

Waraka wa Zamaradi kwa Mobetto, Bifu Lao Lafikia Pabaya!

MTANGAZAJi na mjasiliamali Zamaradi Mketema ameingia ndani ya bifu zito na Mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto Kwenye mitandao ya kijamii huku kisa cha bifu hilo kikidaiwa kuwa ni tuhuma za Zamaradi kuiba idea ya mshono wa nguo yake aliyovaa Kwenye 40 ya mtoto wake wiki chache zilizopita kutoka kwa Hamisa Mobetto kisha kwenda kushona kwa fundi mwingine bila hata taarifa.

 

Baada ya tetesi hizo Zamaradi aliandika Kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa hakuchukua idea ya mshono kutoka kwa Hamisa  bali yeye ndiye alimpa Hamisa mshono lakini alishindwa kushona kwake kutokana na muda.
Zamaradi anaandika;
“Nimeambiwa nilipewa mshono na mtu nikaenda kushona kwingine, na nimeshangazwa na uongo mkubwa wa namna hii, Mimi ndio nimetuma mshono kwake na sio yeye, hakuwa anaufahamu kabla, kutokana na kudai kupishana na muda nikaamua nikashone kwingine na zaidi swala la kushona kokote ni uamuzi wangu since sijachukua mshono wa mtu”.

Baada ya povu hilo la Zamaradi, Hamisa na yeye alimwaga povu zito sana na kuandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwa ameambatanisha message walivyokuwa wanachat:

“First Of All Me sio Mtu wa Kujibishana Na watu insta Ndo maana always nakaaga Kimya ……. Tangia Nimefungua @mobettostyles Kila siku imekua Jipya. Secondly sijawahi Sema Popote kuhusu mshono Wa Shughuli yako wala kuandika kwa My page so probably one of your friends kayapeleka sehemu .

“My dear ulivyokua hujanialika kwenye shughuli yako nilibezwa kuchekwa kutukanwa and all siku jibu wala ongea popote kwasababu kila mtu ana uhuru wa kuchagua watu atakao. 
Ulinitafta Tumechagua Mishono umeenda shona kwengine sijawah lalamika my dear wala kusikitika Coz ridhki mafungu saba na kila likuepukalo najuaga huwa lina kheri na Mtu.

Hivyo basi kama mtu mzima ungeskia kitu ungenifata na kunambia lakin no umeamua kunichafua just because uweze lala vizuri usiku. #MniacheJamani#MaanaNadhanSikuMkinitoaRoho #MtafurahiaSana “

Zamaradi akaandika waraka;
Hata uongo ukinyamanziwa sana huaminika na kuonekana ni ukweli, NAKUJA KUTOA TAMKO SOON juu ya uzushi na uongo unaotembea juu yangu, na hii ni kutokana na jinsi inavyotaka kudisrurb BRAND YANGU na BRAND YA WADHAMINI WANGU ambao ni HAPPIX. Kwa wale wote wanaopenda maanguko yangu na kufurahia uongo unaonendelea ITANENI.

PART 1.

Imenilazimu niongee haya kwa minajili ya kulinda BRAND YANGU na watu NILIOINGIA NAO MKATABA KWASASA hivyo mniwie radhi nitaowakwaza.

Zamani wachawi walikuwa wanajificha wanasubiri giza liingie wapae, ila siku hizi wachawi wamehamia INSTAGRAM wazi kabisa, wanapoona kuna MAFANIKIO, HESHIMA ama MAPENZI kwako watatafuta kila sababu ya KUKUSHUSHA NA KUKURUDISHA CHINI MAKUSUDI kwa kutafuta na kutunga UONGO NA UZUSHI bila uoga wala haya ya kuona wanaongopa, lengo ni kukushusha mfanane, nataka niseme HATUTAFANANA!! Na nimeamua kuongea maana hata UONGO UKINYAMANZIWA SANA HUAMINIKA.

baada ya 40 ya mwanangu kupita, kuna wapuuzi wenye chuki wamejitokeza na kuanza kusema mimi nimechangisha hela ya kufanya 40, na ni kitu kinachosambazwa kwa kasi mno na kutaka kuaminishwa kwa nguvu mpaka inakwaza sasa kiubinaadamu, hivi hii inaingia akilini!!?? kwanza kabisa huo sio utaratibu wangu na kwangu hilo ni swala la aibu sababu sherehe kama ya 40 ni HIARI sio kitu cha lazima.

 

Mwanzoni walisema nimechangiwa na wanakamati kutokana na group la rafiki zangu kwa mapenzi yao kujikusanya kuninunulia ZAWADI YA SURPRISE ambayo ni SETI YA DHAHABU waliyonikabidhi siku ya sherehe, tena sikujua hiko maana hata kwenye group walinitoa ili iwe surprise kwangu, na lengo la group mwanzo ilikuwa ni SARE ila baadae wakanitafutia zawadi kwa mapenzi yao kwangu na jinsi TUNAVYOISHI.

 

Lakini hakuna mwanakamati wala mtu baki hata mmoja aliewahi kunipa hata SHILINGI MIA kama mchango kwangu au kunilipia chochote na SIJAWAHI KUOMBA sababu sio utaratibu wangu na kwenye lile NILIJITOSHELEZA, hivi mmeshindwa kutofautisha ZAWADI NA MICHANGO!?? Sababu tu ya kuona wenzangu wana mapenzi kiasi gani na mimi kuna wengine wanaumia tu na wanabadilisha mada kuwa nimechangiwa, kweli!??

 

Kama niliweza kufanya EVENT ya wanawake wenzangu BURE iliyonicost sio chini ya MILIONI NANE tena bila kusaidiwa na mtu YOYOTE kwa mapenzi tu na kutoa elimu na hawakulipa viingilio leo iweje nichangishe!?? Sio kila mtu ANAPENDA KUJISHAUA NA KUONGEA AMA KURINGISHIA, tusilazimishane tabia zisizo zetu, na nime.

PART 2.

Sio kila mtu ANAPENDA KUJISHAUA NA KUONGEA AMA KURINGISHIA, tusilazimishane tabia zisizo zetu, na nimeongea haya ili tu KULINDA BRAND YANGU inayotafutwa na watu kwa nguvu kutaka kuichafua baada ya maisha yao kuwashinda.

Narudia tena Naongea yote haya not because nataka KURINGISHIA/BRAGGING but because IAM A BRAND, shughuli nzima kabla haijafanyika ilikuwa SPONSORED KILA KITU ULICHOKIONA, HAKUNA ALIENICHANGIA SUMNI YA 40 labda zawadi ambazo zilitoka kwao wenyewe kwa mapenzi yao wenyewe,ukinuliza zimekujaje sijui maana sikuwepo kwenye group zao kujua mipango yao ila naamini ni UTU WAO KWANGU.

Wameona imepita wanaanza kusema kuhusu group nyingine ya watu wa wonder women imenichangia, guys sikumuomba mtu zawadi, wala sijawahi kupiga tarumbeta kusema nataka mtu afanye kitu, watu wamejichanga wenyewe kuninunulia zawadi tena sidhani kama ilizidi elfu 80 tu za KITANZANIA kwa hilo group linalosemwa la watu sio chini ya 200 ambao kwa pamoja ndio hiyo elfu themanini.

 

Sikujua wamepanga saa ngapi wala sikuomba bado naamini ni UTU WAO, kweli sherehe ya sio chini ya MILIONI 20 useme nimechangiwa kupitia hiyo hela ISIYOZIDI LAKI, ukiangalia kuanzia DECOR ambayo @partyboxevents amehusika sio chini ya milioni kumi (invoice attached) chakula, vinywaji, nguo, na kila unachokiona HAKUNA ALIETOA SHILINGI YAKE, tukija kwenye nguo naambiwa nilipewa mshono na mtu nikaenda kushona kwingine!! Funny wallah!!

 

Na nimeshangazwa sana na uongo mkubwa wa namna hii, Nimeattach ushahidi hapo juu kuwa MIMI NDIO NIMETUMA HUO MSHONO KWAKE NA SIO YEYE, hakuwa anaufahamu kabla, hata kama kuna roho mbaya mnanipa sio ya kiasi hiko, sasa hapo nani mbaya!?

 

Kutokana na kupishana na muda nikaona nikashone kwingine, na zaidi Swala la kushona popote ni uamuzi, since sio mshono niliochukua kwa mtu nina uhuru wa kuupeleka popote, nina biashara ya duka la nguo nina CATERING ila silazimishi kila ananenijua aje kwangu, na zaidi SIJISIKII VIBAYA riziki inapoenda kwa wengine, sina roho mbaya hiyo, riziki kugawana. Am very dissapointed kiukweli na binaadamu ila nimegundua kinachofanya haya yote sio kwamba wananihofia mimi ila NGUVU YANGU. hata ukinyamanza kimya watu.

PART 3

Hata ukinyamanza kimya watu watalazimisha ubrag tu hata kama sio tabia yako, kuanzia kila ulichokiona hakuna nilichochangiwa wala kupewa bure, MSIMCHAFUE SPONSOR WANGU ambayo mimi ni BALOZI WAKE, watu walikula, walikunywa na na narudia tena NI PESA YA MFUKONI MWANGU iliyotokana na MDHAMINI WANGU.

 

ALINILIPA ZAIDI YA HIYO NA ACOCOVER COST ZOTE, Na naongea hivi pia kuprotect BRAND ya wadhamini wangu sababu uongo unapitiliza sana, nataka niseme hivi KWA KUJIAMINI. Sijawahi kuomba mchango, kuchangisha wala Kuchangiwa na yeyote kwenye 40 ya mwanangu, na zaidi kama kuna mtu angetaka kunichangia NINGEKATAA bado maana sioni sababu kwenye kitu kama cha kujifurahisha mwenyewe, leo natungiwa maneno kila kona ili tu kunishusha, nawahakikishia SITASHUKA KWA HILO.

 

Na zaidi yeyote alieleta chochote kutoka popote ni ZAWADI AMBAZO SIKUOMBA ila mapenzi ya watu binafsi, sina shilingi kumi ya mtu niliyokula na HAKUKUWA NA HELA YA KULIWA inayoweza kunisaidia kwenye party wala maisha yangu, nawaruhusu kunichukia ila msilazimishe uongo kuwa kweli, kuna tofauti kubwa kati ya ZAWADI NA MICHANGO hivi mimi nina power gani ya kulazimisha watu wachange na wakachanga kwa kuniogopa.

 

Hivi NINAOGOPEWA KIASI HIKO ama NINA NGUVU HIYO!?? Au kuna karama mnayoiona ambayo mimi sijaigundua!?? Kweli jamani!??? Aaaaaah msifanye hivyo, kuna muda kubali yaishe, ZAMU YANGU IMEFIKA.. badala ya kukalia majungu na roho mbaya muombe MUNGU akuone, usiwe busy kushusha watu kwa uongo na uzushi na kuwachafua ama kuwatukanisha HAITAKUPANDISHA WEWE!! Sana sana unajibebea laana za kushindwa kuendelea, hata MBELE ZA MUNGU hafurahii.

Nisameheni niliowakwaza, nililazimika kuliweka hili sawa sababu lilitaka kuathiri hadi brand ya wengine ninayoisimamia mimi. MNIWIE RADHI.

Kila ninavyozidi kukua ndio napata jibu kwanini hata MITUME walizomewa na kupigwa mawe haliyakuwa walitangaza neno la KWELI LA MUNGU 😊 #amanimoyoni

The post Waraka wa Zamaradi kwa Mobetto, Bifu Lao Lafikia Pabaya! appeared first on Global Publishers.