NEWS

17 Agosti 2018

Zamaradi Aongelea Swala la Dina Marious


Mwanadada Zamaradi Mketema amefunguka na kujibu tuhuma alizokuwa akizsudhiwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya page za udaku kuwa yeye ndui chanzo kikubwa cha Dina Marious kufukuzwa kazi Clouds media na kuanza kutafuta kazi sehemu nyingine.

Wakati Dina na Zamaradi wakifanya kazi clouds , walikuwa marafiki hapo mwanzo lakini dina alikuja kusikika ameacha kazi clouds ilikuja kusemekana kuwa kuna vitu vya chini chini vilikuwa vikiendelea kati ya dina na zamaradi vilivyosababisha mwanamama huyo kufukuzwa kazi.

Hata hivyo akiongea na bongo 5, Zamaradi anasema kuwa haiwezekani kuwa mahusiano yake na mkurugenzi wa vipindi clouds media usababishe kufukuzwa kwa Dina, huku akihoji kama Dina aliwahi kuwa mke mwenzie.

Kuhusu Dina Marious , sikuwahi kugombana nae wala sikuwahi kuambiana nae mjinga au mjinga mwenyewe wala nini, na kwa mtu mwenye akili kubw unaweza kukaa ukawaza kuwa kwa mtu kama mimi ambae nilikuwa tu mtangazaji , ninawezaje kumfukuzisha mtu kazi.

Siwezi kumlaumu mtu yoyote lakini ndio hivyo siku zote mti wenye matunda ni lazima utapigwa mawe.

Hata hivyo alipoulizwa kuwa sababu kubwa ni kwa kuwa yeye kipindi icho alikuwa na nguvu kutokana na kuwa na mahusiano ya kimapenzi  na bossi ruge, ndipo zamaradi alipohoji ” kwani mimi Dina alikuwa mke mwenzangu “